Teddy Kilanga Arusha.

Wadau wa kutetea haki za watoto mkoani Arusha pamoja na vyombo vya dola wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika ulinzi wa mtoto na uwezeshaji wa vijana katika  uhimarishaji wa familia.



Amesema hayo Mkuu wa wilaya ya Karatu,Dadi Kolimba katika uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa shughuli za utendaji kazi wa shirika lisilo la kiserikali la kulea watoto na vijana katika kutoa elimu na afya pamoja na hupatikanaji wa haki (SOS) uliyofanyikia jijini Arusha ambapo ameelekeza kuhimarisha umoja wa ulinzi wa mtoto katika familia.



"Naomba nitoe maelekezo kwa wadau wote wakiwemo wazazi,walezi jamii,Taasisi za dini,Asasi za kiraia,serikali  za mitaa,vyombo vya dola kushirikiana kwa pamoja  katika ulinzi wa mtoto na uwezeshaji wa vijana na uhimarishaji wa familia,"amesema Kolimba.



Aidha amesema serikali mkoani Arusha inatambua mchango mkubwa unaofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya mia sita yaliyosaidia juhudi za serikali katika sekta za afya ,elimu,maendeleo ya jamii na nyinginezo.



Kolimba amesema ni matumaini yake ufadhiri huo wa mradi wa upanuzi wa shughuli za SOS katika wilaya hizo zitawafikiwa watoto, vijana na familia  zilizotangulia katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha hivyo ni mategemeo ya serikali na uongozi wa mkoa wa Arusha na jamii nzima pamoja na uongozi wa SOS watahakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa watoto wa vizazi vijavyo.



Alisema shirika hilo la SOS limekuwa mdau mkubwa katika kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa sera  mbalimbali zinazowezesha kutimiza malengo ya kuwahudumia watoto na familia zilizokatika mazingira hatarishi katika mkoa wa Arusha,Mwanza,Dar es Salaam,Iringa na Visiwani Zanzibar.



Kwa upande wake Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa Arusha,ACP.Happiness Temu ameshukuru shirika la SOS kwa kuendelea kupunguza kasi ya uwepo wa watoto wa mitaani katika kutatua baadhi ya changamoto zinazowakumba watoto wanaoishi katika mazingira magumu.



Dkt Nandera Mhando kutoka Ofisi ya Tamisemi amesema SOS imekuwa mfano kwa NG'O zingine pamoja na wadau wengine katika kusimamia kazi ya kutoa watoto wanaoishi mitaani na kuwaunganisha na familia zao.



Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda amesema ni vyema serikali kwa kushirikiana na jamii  wakasimamia maendeleo ya watoto kwa vitendo zaidi.



Naye Mwenyekiti wa bodi ya shirika la SOS, Haruni Masebu amesema lengo la mradi huo ni kuwezesha kumlinda mtoto katika kutoa malezi mbadala na kuhakikisha watoto wanaopitia changamoto za ukosefu wa malezi wanakuwa na matumaini mapya katika kukua kwenya mazingira ya familia yenye upendo,heshima na yenye ulinzi.



Mwenyekiti huyo amesema ili kupanua wigo wa wakumlinda mtoto na kuhakikisha kuwa anakua katika mazingira bora na kuheshimiwa wameongeza huduma na kufikiwa halmashuri nne ikiwemo jiji la Arusha,halmashauri ya Arusha,Meru na Karatu.



"Pamoja na hilo kuna baadhi ya changamoto ambazo shirika limekumbananazo  ikiwemo wananchi kuchukulia shirika hili kama kitengo cha kutoa fedha hivyo kupelekea upotoshaji wa lengo mahususi la kusaidia watotoa waliokatika changamoto za malezi hivyo tunaiomba serikali kuendelea kushirikiana nasi katika kutoa elimu kuhusiana na sheria ya mtoto kupitia miongozo mbalimbali,"amesema.

Share To:

Post A Comment: