• Wateja watapata hadi  GB 78 za intaneti bila malipo kwa mwaka mzima.


Dar es Salaam. Tarehe 5 Aprili, 2022. Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za  kidijitali Tanzania, Tigo Tanzania, imeshirikiana na INFINIX Tanzania kuzindua INFINIX SMART 6 ambayo itauzwa kwa bei ya shilingi 220,000 na HOT 12i kwa Tsh 270,000. Akizungumza katika uzinduzi huo , Mtaalam wa Bidhaa za  Intaneti kutoka Tigo, Blass Abdon amesema kuwa 

“Tunafuraha tena kuungana na INFINIX Tanzania kuzindua simu mpya za kisasa ambazo zitaimarisha zaidi lengo letu la kuunganisha watanzania katika mfumo wa huduma za Kidigitali  kote nchini. Na Mfumo huu unaimarisha zaidi imani ya washirika wetu hasa katika mtandao wetu wa 4G  uliosambaa kote nchini”.

“Kulingana na mkakati wetu wa kuharakisha kupenya kwa simu za kisasa nchini huku tukihakikisha kuwa wateja wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa GB 78 za intaneti BURE kwa muda wa mwaka mmoja  kwa wateja wote watakaonunua simu janja za Infinix Smart 6 na HOT 12i.” alisisitiza Abdon. Naye kwa Upande wake Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema kuwa “Leo tumetangaza kuzindua simu mpya kabisa ya Infinix HOT 12i, simu mahiri mpya ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu  kama zilivyo simu zetu siku zote, Infinix ina RAM ya kutosha, teknolojia ya fusion huruhusu simu za HOT 12i kuongeza RAM Mfano  3GB ya RAM inaweza kuongezwa mpaka kuwa 6GB ya Ram, Screen kubwa ya 6.6HD+" 90Hz Pro-Level ya elektroniki itakayokufanya ufurahie kucheza Game katika simu yako. Pia Inakuja na betri ya 5000mAh, Chipset Helio, itakayokufanya utumie simu yako katika masuala mbalimbali kama kucheza game , kuingia kwenye mitandao ya kijamii na mambo mengine mengi bila kuhofia chaji kuisha”,

“Tumejitolea daima kubuni simu mahiri zenye utendakazi bora na za kisasa kwa wateja wetu, huku zikiwa mpya zenye ubora wa hali ya juu na gharama nafuu kila wakati. Infinix HOT 12i na Smart 6 zimepata mafanikio katika utendakazi ulioboreshwa, ustahimilivu wa muda mrefu, muundo wa kisasa wa Smart 6  huku zikihakikisha ulinzi thabiti .

Tunawakaribisha wateja Wetu wote katika maduka ya Infinix na Tigo Nchini kujipatia simu hizi mpya na za kisasa na kufurahia maisha ya Kidigitali ". Alimalizia Aisha Karupa.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: