Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Watu sita (06) wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyo husisha gari Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameseama ajali hiyo imetokea tarehe 19.04.2022 muda wa saa nne usiku na  kuyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu  na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva amabapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiri waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

ACP Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha

Share To:

Post A Comment: