Na  Mustafa  Leu.

MKEMIA  mkuu ni kikwazo cha mtafiti kupata mafanikio ya tafiti zake na kusababisha bidhaa anazozalisha kushindwa kuwepo kwenye masoko na kushindwa kupata mafanikio na malengo ya ufafiti wake.

Kwa kipindi cha miaka 40 ya utafiti pamoja na kuwasilisha matokeo ya tafiti zake ofisi ya Mkemia mkuu imeshindwa kutoa Kibali cha kuidhinisha kwa dawa zilizofanyiwa utafiti kwa kutumia teknolojia ili ziingie kwenye soko.


Hali hiyo inamfanya mtafiti Salvatory Rwebangira,mwenye umri wa miaka( 72) analazimika kusubiri mamlaka husika ili iweze kuidhinisha dawa zake anazozalisha  bila kutumia kemikali ili ziweze kuingia kwenye masoko na kutumika kutibu magonjwa mbalimbali..

Amesema kuwa miaka 40 imepita tangia aanze kufanya utafiti wa dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ameambulia kutunukiwa cheti cha kutambuliwa dawa zake kutoka Muhimbili   Medical research lakini hakimwezeshl kupeleka dawa zake kwenye masoko mpaka apate kiballi toka kwa mkemia mkuu wa serikali..

Rwebangira,anasema kuwa mara baada ya yakukamilisha tafiti za dawa ambazo anaamini zina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali miaka michache iliyopita aliwasilisha aina 30 tafiti  zake kwa mkemia mkun na. taasisi ya utafiti wa tiba asili taa mhimbili ili wazipitie na hatimae ziidhinishwe bado hajakata tamaaa.

Rwebangira,anasema katika kipindi hicho cha muda wa miaka 40 amekuwa akifanya tafiti ambapo ameweza kutengeneza bidhaa zisizo na kemikali zikiwemo dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ambayo ni mtoto wa jicho uoni hafifu ,kutoona mbali au karibu,kutosoma maandishi.

Anasema ametengeneza mafuta yanayotokana na wanyama ,miti, asali ,na ametengeneza sabuni,alianzisha maabara yake inayotembea mjini Mwanza ,ambayo sasa ameihamishia  nyumbani kwake maeneo ya uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.

Anasema safari yake ya utafiti wa dawa ilianza mwaka1977 baada ya Wazungu waliokuwepo nchini wakifanya kazi na kaka yake walipokutana nae na kumshauri kaka yake ampeleke nchini Uganda kufundishwa utafiti wa dawa na madini mafunzo  ambayo yalimchukua miaka minne.

Anasema alipokuwa shuleni hakuwahi kuwa na wazo la kuwa iko siku atakuwa mtafiti ,wazo hilo lilikuja kutokana na kuhamasishwa na wazungu ambao walikuwa ni rafiki wa kaka yake waliokuwa wakifanya nae kazi ya utafiti ambao baada ya kumuona na kuhojiana nae waligundua kuwa ana kipaji cha kufanya utafiti

Mwaka 1994,baada ya kuhitimu mafunzo yake alirejea nchini na kupokelewa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojiamCOSTECH, ambapo aliwasilsha  tafiti zake mwaka1997  na chuo kikuu cha Dar es Salaam,kilithibitisha teknolojia yake ya utengenezaji wa wadawa aliyokuwa akiitumia kufanya ugunduzi utafiti wake


Anasema COSTECH, imeendelea kumfadhili hadil eo ambapo bado anaendelea na utafiti na tayari ameshaanza kuwashirikisha watoto wake huku baadhi ya wajukuu wake ambao  bado ni wadogo nao wameonyesha nia ya kujiunga na utafiti wa dawa.

Anasema ana uwezo wa kuzalisha vikinga maambukizi ya ugonjwa wa Uviko19  (Santizer,) za kutosheleza mahitaji ya nchi nzima bado anasubiri kibali cha mkemia mkuu wa serikali

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: