Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na kufanya  mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Donald J. Wright na ujumbe wake leo Aprili 05, 2022 Jijini Dodoma.


Katika mazungumzo hayo Wamejadili masuala mbalimbali ya kukuza ushirikiano katika Sekta ya elimu, afya na fursa za kubadilishana taaluma ya elimu kwa wanafunzi kwenda na kuja kusoma katika nchi hizo mbili.Pamoja na mambo mengine, Wamejadili vipaumbele vya maaendeleo ambavyo nchi ya Marekani inaweza kusaidiana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo mara nyingi misaada ya wahisani huangalia vipaumbele vya mtoaji na siyo mhitaji.

Share To:

Post A Comment: