Na Ahmed Mahmoud

MAKAMU Mwenyekiti wa Chaka cha Mapinduzi CCM,bara, Komredi Abdalahamani Kinana, amewasili leo mkoani Arusha akitokea mkoani Kilimanjaro na kupokelewa na Viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama na serikali na wanachama wa CCM.

Akizungumza na. wanachama wakati wa mapokezi hayo yaliyofanyika ofisi kuu ya ccm,mkoa, Kinana,amepongeza mapokezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa wanachama,viongozi na wananchi.

Amesema Mara Banda ya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa ccm,ameanza ziara za amshaamsha ndani ya Chama ambayo ameianzia mkoa wa Dar,es Salaam Pwani, Tanga na. Kilimanjaro  na leo amefikaArusha.

Amesema kesho atazungunza na wanachama wa Chama cha mapinduzi mkoa kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru

Leo jioni Kinana atashiriki kwenye IFtari ambayo imeandaliwa kwenye ukumbi wa Chama cha mapinduzi ccm,mkoa wa Arusha.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: