Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Usimamizi wa Hakimiliki, Bw.Philemon Kilaka (katikati) akiwa pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMA JKT Meja Jamal Mohamed (kulia) wakisaini mkataba wa ukusanyaji wa mirabaha katika mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma , hafla iliyofanyika leo Aprili 13,2022 kwenye ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Usimamizi wa Hakimiliki, Bw.Philemon Kilaka (kushoto) akiwa pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMA JKT Meja Jamal Mohamed wakionesha mkataba walioingia wa ukusanyaji wa mirabaha, hafla iliyofanyika leo Aprili 13,2022 kwenye ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Usimamizi wa Hakimiliki, Bw.Philemon Kilaka akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ukusanyaji wa mirabaha na kampuni ya SUMA JKT Auction Mart Ltd, hafla iliyofanyika leo Aprili 13,2022 kwenye ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Usimamizi wa Hakimiliki, Bw.Philemon Kilaka (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ukusanyaji wa mirabaha na kampuni ya SUMA JKT Auction Mart Ltd, hafla iliyofanyika leo Aprili 13,2022 kwenye ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam. Mwanasheria COSOTA Bw.Zephania Lyamuya akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ukusanyaji wa mirabaha na kampuni ya SUMA JKT Auction Mart Ltd, hafla iliyofanyika leo Aprili 13,2022 kwenye ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMA JKT Meja Jamal Mohamed akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ukusanyaji wa mirabaha na kampuni ya SUMA JKT Auction Mart Ltd, hafla iliyofanyika leo Aprili 13,2022 kwenye ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI ya Hakimiliki (COSOTA) imeingia mkataba na Kampuni ya SUMA JKT Auction Mart Ltd kwaajili ya ukusanyaji wa mirabaha katika Mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma ambapo mkata huo ni wa mwaka mmoja kuanzia leo Aprili 13,2022.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Usimamizi wa Hakimiliki, Bw.Philemon Kilaka amesema utaratibu wa kukusanya na kugawa mirabaha umekuwa ukifanyika sehemu mbalimbali Duniani na katika maeneo mbalimbali ya biashara yanayotumia kazi za muziki na filamu.

"Katika kuhakikisha wasanii wananufaika na matumizi ya kazi zao katika maeneo mbalimbali ya kibiashara COSOTA inaendelea kuingia mikataba na mawakala katika sehemu mbalimbali ili kuhakikisha inaongeza makusanyo kwa kufikia maeneo mengi". Amesema Bw.Kilaka.

Aidha Bw.Kilaka amesema imeomba mawakala hao kupewa ushirikiano kote watakapopita na mawakala hao watatambulika kwa vitambulisho vilivyotolewa na COSOTA pamoja kwa upande wa mawakala kutoka SUMAJKT watatambuliwa kwa vitambulisho vya ofisi yao.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa watumiaji wa kazi za muziki na filamu nchini katika maeneo ya kibiashara kuhakikisha wanalipia matumizi ya kazi hizo COSOTA ili kuepusha usumbufu pale zoezi la operesheni ya ukaguzi litakapofanyika.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya SUMA JKT Meja Jamal Mohamed amesema kampuni hiyo imekuwa na uzoefu mkubwa katika ukusanyaji wa mapato hivyo amewataka wananchi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa jukumu hilo.

"Kazi za sanaa ni kazi kama aina nyingine za kazi katika kutafuta vipato, wasanii wanatumia akili zao, nguvu zao na muda wao katika kuandaa kazi zao hivyo nao wanahaki ya kufaidika kama wanavyofaidika watu wengine wanaofanya shughuli za uzalishaji mali". Amesema .

Hivyo basi amesema watahakikisha kazi hiyo wanaifanya ipasavyo na kwa kufuata sheria, kanuni na utaratibu mbalimbali zinazoongoza nchi hii.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: