Na Ahmed Mahmoud

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia,barani Afrika Nelson  Mandela, imekuja na ugunduzi wa kutibu majitaka na kuyatumia kwa kilimo sanjari na kufungua milango kwa baadhi ya watafiti na wagunduzi wa kisayansi ambao tafiti zao hazijafikishwa kwenye taasisi husika.
Aidha Tafiti hizo ni sehemu ya ufadhili kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kufanya tafiti na Ubunifu ambazo ni kipaumbele cha serikali ambazo watafiti hawajazifikisha eneo husika kutokana na sababu mbalimbalii kuwasilisha tafiti zao kwenye taasisi hiyo.

Hatahivyo Chuo hicho kimekuja na ugunduzi wa kuyabadilisha matumizi ya majitaka na kutumika katika kilimo cha ndizi sanjari na kuzalisha biogesi kuweza kuzalisha umeme.

Hii inakuwa ni taasisi ya kwanza ya Wabobezi wa Sayansi na teknolojia barani Afrika kufungua milango kwa  watafiti  kuitumia taasisi hiyo kuwasilisha tafiti na gunduzi zao lengo ni kuwaendeleza kwenye tafiti zao
Makamu mkuu wa taasisi hiyo Profesa Anthony Mshandete,anasema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo zimechangia baadhi ya watafiti kushindwa kuwasilisha tafiti zao na hivyo matokeo ya tafiti zao kuto tambulika kutokana na changamoto hiyo taasisi imefungua milango  kwa watafiti hao .


Akizungumza na baadhi ya  wanahabari na watafiti na wabunifu wa kanda ya kaskazini waliopata mafunzo ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ,ofisini kwake kuhusu hatua zinazochukuliwa na taasisi hiyo kuwaendeleza watafiti mbalimbali,Profesa Mshandete, amesema taasisi hiyo inathamini Kazi za utafiti na ugunduzi ili ziweze kuleta maendeleo ya haraka.

Ameeleza hiyo ni fursa kwa watafiti nchini ambao walishafanya utafiti na kufanya ugunduzi lakini tafiti zao hawajaziwasilisha kwenye taasisi za kisayansi ili ziweze kutoa matokeo yanayosubiriwa ili zinufaishe  umma.

Kutokana changamoto hiyo Taasisi hiyo imeamua kufungua milango na kuwaalika  watafiti walipo nje ya mfumo  kuwasilisha utafiti na ugunduzi zao na kuwezesha kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye nyanja ya utafiti

Watafiti na wabunifu ni muhimu  katika maisha ya sayansi  kwa kuwa sayansi inaamini katika ugunduzi,utafiti,na namba ambazo hutoa matokeo halisi.

Kwa mujibu wa Profesa Mshandete,katika kuendeleza na kuhamasisha maswala ya kutafiti na ugunduzi ,Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH,) imefadhili taasisi hiyo ili kuendeleza na kukuza teknolojia ya sayansi na utafiti nchini.Anabainisha kwamba taasisi hiyo inawaibua watafiti na wagunduzi wasiofahamika na kuwaweka mbele kutokana na. kutambua na kuthamini shughuli zao lengo ni kuongeza idadi ya  watafiti kuwa wengi

Kwa muktadha huo Serikali kupitia chuo hicho wamejipanga kuhakikisha Tafiti Ubunifu na ugunduzi zinapewa kipaumbele ili kuinufaisha jamii na Utafiti huo kwa Lengo la kuleta tija katika uzalishaji wa bidhaa na mazao.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: