Viongozi wa Kanisa la Anglikan wilayani  Monduli Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuweka mikakati endelevu kwaajili ya kujiingizia mapato yake tofauti na kumtegemea Sadaka za waumini.

Ushauri huo ulitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Monduli Robert Siyantemi alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Bw,Frank Mwaisumbe katika Changizi lililoandaliwa kwaajili ya ujenzi wa Kanisa hilo.

Alisema kuwa Kanisa linatakiwa kuwa na mipango endelevu hasa kujitegemea katika kufungua miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Shule,Hosteli ama Ufugaji kwani kwa kufanya hivyo watapata mapato mengine yanayoweza kuendeleza shughuli mbalimbali za Kanisa hilo.


"Mtafute eneo kubwa kupitia Halmashauri yetu ya Monduli na Ofisi ya Mkuu ya Wilaya iko tayari kuwapa Wataalamu waliobobea katika kuandika maandiko na kulishauri Kanisa  ni mradi upi wenye tija ndani ya Wilaya yetu"aliongeza kusema


Awali akisoma risala kwa mgeni Rasmi,Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi katika Kanisa hilo Bi,Jane Kimweri alisema moja ya changamoto inayolikabili Kanisa hilo kushindwa kuendelea ni pamoja na ufinyu wa fedha kwaajili ya kumalizia ujenzi wa Kanisa pamoja na wakristo kuendelea kupungua siku hadi siku kukwepa majukumu ya ujenzi.


Bi Kimweri pia alitaja matarajio ya Kanisa hilo kuwa ni pamoja na kumaliza ujenzi wa Kanisa sehemu iliyobaki ambayo ni kupiga plasta kuta zote ndani na nje,kutandika vigae na terezo chini,kuweka milango na madirisha pamoja na kujenga nyumba ya mtumishi.


Katika Harambee hiyo Shilingi Milioni 18 zilitarajiwa kukusanywa ambapo jumla ya shilingi Milioni 6,700,000 zilikusanywa ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslimu.

Share To:

Post A Comment: