Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka watumishi wa Mamlaka ya Maji wilayani Maswa mkoani Simiyu kupendana ili waweze kufanya kazi zao kwa moyo mmoja na hatimaye kuwakwamua wananchi na kero ya maji inayowakabili.


Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa Rai hiyo wilayani Maswa wakati akikagua na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambao umejengwa na watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Maswa kwa mtindo wa force account.


Amesema ili miradi ya maji vijijini kote nchini itekelezwe kwa mafanikio makubwa ni lazima watumishi wa Mamlaka za maji Vijijini, (RUWASA) wapendane na kuaminiana kuanzia watumishi wa chini mpaka kwa mabosi wao ili waweze kufanya kazi kama timu moja.


Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Maswa, mhandisi Nandi Mathias amesema ujenzi wa mradi huo wenye gharama za zaidi ya shilingi milioni 800 unahusisha ujenzi wa tenki kubwa  lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja kwa siku na miundombinu mingine ya kupeleka maji kwa wananchi.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Maswa.


Kwa upande wake Mbunge wa Maswa, Mhe. Stanslaus Nyongo ameipongeza Serikali kwa kuwaondolea wananchi wake kero kubwa ya upatikanaji wa maji ambayo imewatesa kwa miaka mingi.
Share To:

Post A Comment: