Mkuu wa Wilaya ya lushoto Kalisti Lazaro amepiga marufuku kutumia mafundi ujenzi kutoka nje  ya Tarafa  ya Mgwashi  katika ujenzi wa upanuzi wa Kituo Cha  Afya kinachojengwa mjini humo.


Agizo hilo amelitoa wakati wa hafla ya kutambulisha na kukabidhi mradi wa upanuzi wa Kituo Cha afya Mgwashi kilichopewa sh. Million 500 na serikali ya awamu ya sita.


Mkuu huyo wa Wilaya alisema fedha hizo zitajenga majengo matano ikiwemo jengo la Mama na Mtoto.


"Naagiza upanuzi huu ufanywe na mafundi kutoka ndani ya Tarafa ya Mgwashi badala ya mafundi kutoka nje ya Tarafa hii nikikuta mafundi wa nje kutoka Bumbuli,Lushoto ,Moshi na maeneo mengine  nitawaondoa "Alisisitiza  Mkuu huyo wa Wilaya 


Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa hatarajii fundi atoke nje ya Tarafa ya Mgwashi nakwamba endapo atakuta fundi kutoka katika maeneo mengine atamtimua huku Akieleza Kituo hicho kitasaidi Wakazi wa maeneo hayo na maeneo jirani.


Alisema kuwa kukamilika Kwa upanuzi  huo wa Kituo utasaidia kupatika Kwa huduma zote zilizokuwa hazipatikani awali .


"Tunaishukuru Serikali yetu Kwa kutupatia milion 500 za upanuzi  wa ujenzi wa Kituo hiki" Alisema  nakuongeza kuwa lengo la Rais Samia ni kuboresha huduma za afya ikiwemo huduma ya mama na mtoto nchini.


Aliongeza Kwa kusema anatarajia Kituo hicho kitakuwa Cha kisasa na wananchi watapata huduma bora na za kisasa..Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wajitokeze katika kusaidia nguvu kazi ili Kituo hichi kikamilike Kwa wakati lakini pia itasaidia kupunguza matumizi ya fedha nakwamba hata zikibaki zitumike Kwa mahitaji mengine.


Maliwaza Ally ni Mkazi wa Kijiji Cha Wanga alisema kuwa upanuzi huo utawasaidia kupata huduma karibu hasa wakati wa kujifungua sababu waliokuwa wanalazimika kwenda kwenda umbali mrefu kufuata huduma za upasuaji kitu ambacho alisisitiza ni atari Kwa afya ya mgonjwa.


"Kulikuwa hakuna vyumba vya upasuaji,vyumba vya wagonjwa , OPD ilikuwa ndogo  na chumba Cha upasuaji kulikuwa hakuna" Alisema Yahaya Sangoda ambaye zamani alikuwa muuguzi" Alisema Sangoda


Mkazi mwingi wa Mgwashi zainabu Shemdoe Alisema kupandishwa hadhi Kwa Kituo hiki kitasaidia kuokoa vifo Kwa wajawazito na watoto .


Hata hivyo Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Kelvini Shukia Alisema awali kulikuwa na changamoto za kukosekana Kwa vipimo vikubwa hivyo anaamini Kwa upanuzi huo unakwenda kupunguza changamoto hizo.


Share To:

Post A Comment: