Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam, Jumatano ya 30, 2022 Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali na  yenye watumiaji zaidi ya milioni 13 wanaotumia huduma zake Tigo Tanzania, leo imeshirikiana na Dunia Investment kuzindua mchezo wa bahati nasibu kupitia simu ya mkononi iitwayo "DILIPESA" ya zawadi na burudani papo hapo kwa wateja wa Tigo Pesa.

Madhumuni ya huduma ni kuongeza kiwango cha juu cha ushirikiano na kupenya kwa huduma za kifedha kati ya wateja wake, kwa kutumia njia ya michezo.


Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Masoko kutoka Dunia Investment Limited, Bwana Kumesan Pather alisema “Tunajivunia kutambulisha DILIPESA na kuwaletea uzoefu usio na kifani wa michezo, zawadi na Ushindi. Mtu yeyote anayetumia Tigopesa sasa ataweza kujihusisha na huduma yetu na kufurahia ofa za ubunifu na za kuridhisha za mchezo.


Huduma hii ni bure bila malipo yoyote na itapatikana kupitia menyu ya Tigopesa *150*01#, kwa bei ya chini kama TZS 500, nchini kote kwa Kiingereza na Kiswahili.

Pia, kwa kuzingatia mapenzi ya Tanzania katika Soka na Michezo, pia tumeweka SOKA LIVE kwenye toleo letu la uzinduzi wa Wapi Simba? (iko wapi Simba), Dodo x36 (surprise 36) na Jackpot Leo, ambayo ni Jackpot ya Kila siku.


Tunaamini wateja wengi zaidi wa Tigopesa watafurahia programu hii. Na wale ambao bado hawajasajiliwa, watajiunga pia ili kufurahia manufaa” aliongeza Kumesan.

Kwa upande wake Meneja  wa biashara-Tigo Pesa ,. Fabian Felician, alisema “Ilikuwa furaha sana kwetu kufanya kazi na Dunia Investment  na Axieva kuendeleza huduma hii ya kusisimua. Kwa kutumia Dilipesa, wateja wa Tigo sasa wataweza kufurahia vivutio vya kipekee, zawadi na ofa za kushtukiza kwa kujihusisha na huduma yetu ya kifedha ya TIGOPESA. Ikiwemo nafasi ya KUSHINDA Pikipiki, Kompyuta za mkononi, Simu na Tiketi za Kusafiri; pia watakuwa na chaguzi za kuingiza hadi Mamilioni ya Shilingi kila siku.


Yote inategemea mtumiaji, jinsi anavyotaka uzoefu wake wa matumizi ya Dilipesa, ambayo hufanya kazi kwenye simu na kwa urahisi,” alisema Felician.

Uzinduzi huo pia uliambatana na uwepo wa viongozi kutoka bodi ya udhibiti, akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. James Mbalwe; ambaye alipongeza ushirikiano huo na kusema kuwa  “Tunafuraha kuona ushirikiano huu wa kibunifu wa Dunia na Tigo na Axieva ili kuendesha ushiriki wa huduma za Kifedha kupitia Michezo iliyochanganyika.


Huu ni mpango mzuri na Dunia imekuwa mwendeshaji anayeaminika katika soko hili.


Tunatumai uzinduzi huu utapokelewa vyema na wateja na kufungua njia kwa tasnia hiyo kufuata na kuendesha ubunifu zaidi kama huu,” alitoa maoni James.


Uzinduzi wa ushirikiano huu umetegemea sana teknolojia, utafiti na kazi ya utekelezaji iliyofanywa na Axieva; moja ya kampuni zinazoongoza za jukwaa la Fintech katika kanda.


Akizungumza kwa upande wake Bw. Avnish Bhatt, Mkurugenzi wa Mauzo katika Axieva Africa alisema, “Tuna bahati kuwa sehemu ya mpango huu,  Uzinduzi wa leo na Tigopesa unaenda pamoja na dira yetu ya kupenya kwa ujumuishi wa huduma za Kifedha.


Pia tunapenda kuwashukuru Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, kwa uwezo wao wa kuona mbele, vibali na mwongozo wao ambao bila hiyo uzinduzi wa leo wa ‘Gamification of Financial Services’ usingewezekana”.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: