Mwenyekiti wa Kamati hiyoziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka katikati akizungumza wakati wa ziara yao kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Athanasius Nangali akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Athanasius Nangali kulia akisisitiza jambo kwa kamati hiyo



NA OSCAR ASSENGA,KOROGWE.

SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limesema maandalizi ya utekelezaji wa mpango mkubwa wa ukarabati wa kituo cha kuzalisha umeme cha Hale kilichojengwa miaka 58 iliyopita yameelezwa kuwa katika hatua ya juu.

Hayo yalibainishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Athanasius Nangali wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa taratibu zote za manunuzi ziko katika hatua nzuri.

Alisema kuwa mpango huo wa ukarabati unalenga kuleta mabadiliko kukifanya kituo hicho kuwa cha kisasa kinachotumia technologia ya kisasa.

Aidha alisema kituo hicho kilijengwa mwaka 1964 na sasa hivi kinazalisha chini ya megawati 10 kati ya uwezo wake wa kuzalisha megawati 21 huku ikielezwa kuwa ni turnine moja tu inayofanya kazi kwa sasa kati ya turnine mbili zilizopo hapo.

Nangali alisema katika ziara ya Kamati hiyo ya Mahesabu ya Serikali ilikuwa muhimu sana kwa mpango wa kampuni wa kutekeleza mradi wa kufufua mtambo huo ili ufanye kazi kwa uwezo wake wote.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka alisema kamati imeona na kujiridhisha juu ya umuhimu wa ukarabati mkubwa na mtambo wa kisasa.

Alisema ziara yao inalenga kujiridhisha iwapo gharama za mradi zinazopendekezwa zilikidhi vigezo vya thamani ya fedha.

“Tumeona haja ya kugeuza mtambo huo kuwa mtambo wa kisasa wa kuzalisha umeme kwani bado kuna masuala ya fedha hayajakamilika na tumewaita Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme na Afisa Mtendaji Mkuu kwenda Dodoma ili kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na kamati,” Alisema.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: