Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah (kushoto) akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua jengo la mionzi (X-RAY) katika Hospitali ya Sokine iliyopo Manispaa ya Singida  jana. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Mjini Ally Mwendo na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Sokoine, Dk. Asha Byantungama.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la mionzi la kituo cha Afya Sokoine.
Muonekano wa Jengo la Mionzi la Kituo cha Afya cha Sokoine.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Sokoine, Dk. Asha Byantungama akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Anwar Milulu. akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa jengo hilo.
Diwani wa Kata ya Misuna , Hamisi Kisuke akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa jengo hilo.



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Singida, Mhandisi Patrick Zamba (kushoto) akitoa taarifa kwa wajumbe wa kamati hiyo.

Muonekano wa tenki la kuhifadhia maji kwenye mradi huo.



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Singida, Mhandisi Patrick Zamba akisisitiza jambo kwa wajumbe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah (kulia) akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua mradi huo wa maji.
Muonekano wa majengo ya Kituo cha Afya cha Mandewa.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua ujenzi waKituo cha Afya Mandewa.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Anwar Milulu (katikati) akitoa maelezo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mandewa kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Ukaguzi wa kituo hicho cha Afya ukiendelea.
Katibu wa CCM Kata ya Mandewa, Yusuph Kijanga akizungumzia mradi huo ambapo  aliishukuru Serikali hasa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa Kituo hicho cha Afya ambacho kikikamilika kitawapunguzia adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kwenda Kituo cha Afya cha Sokoine kupata matibabu. .
Diwaniwa Kata ya Mandewa Hamisi Baraka akichangia jambo wakati wa ukaguzi wa mradi huo ambapo aliomba wasaidiwe kujengewa barabara za kufika katika kituo hicho cha Afya.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua ujenzi wa Zahanati ya Ititi.
Muonekano wa moja ya Jengo linalojengwa la Shule ya Sekondari ya Uhamaka.
Muonekano wa moja ya Jengo linalojengwa la Shule ya Sekondari ya Uhamaka.
Msimamizi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Uhamaka Mwalimu Georgia Maghiya (kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo kwa kamati hiyo.
Ukaguzi wa ujenzi wa vyoo vya shule hiyo ukifanyika.

Ukaguzi wa majengo ya shule hiyo yanayo jengwa ukifanyika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Alhajj Juma Killimbah akiongoza ukaguzi huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Alhajj Juma Killimbah akisisitiza jambo wakati wa  ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo.Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida mjini, Lusia Mwiru..
Diwani wa Kata ya Uhamaka, Senge Masidi Senge akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenziwa shule hiyoya Sekondari ambapo alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha za ujenzi huo.
Mwananchi wa Kijiji cha Uhamaka Daniel Kanka Senge akishukuru Serikali kwa kusaidia kujenga shule hiyo. 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


MKUU wa Mkoa Singida Dk.Binilith Mahenge amesema Serikali imeridhia majengo ya iliyokuwa  Hospitali ya Mkoa wa Singida kuwa Hospitali ya Wilaya ya Singida.

Dk.  Mahenge aliyasema hayo jana wakati kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida ilipokuwa ikikagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Manispaa ya Singida. 

"Serikali tayari imekwisha ridhia majengo hayo kuwa Hospitali ya Wilaya baada ya kukubaliana pande zote   Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI), Wizara ya Afya, Mkoa na Wilaya" alisema Mahenge.

Alisema suala lililokuwa bado ni idadi ya majengo yatakayochukuliwa ambayo ni saba ya na sasa jambo linalosubiriwa ni Wizara ya Afya kuwaandikia barua TAMISEMI ya kuwakabidhi majengo hayo.

Wakati huo huo Dk.Mahenge ameiagiza Manispaa ya Singida kutoa haraka fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la mionzi (X-RAY) katika Kituo cha Afya cha Sokoine ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah alisema wameridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

"Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza," alisema Kilimbah.

Kilimbah alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii badala ya kuisubiri Serikali.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Aliwaomba wananchi kila ilipotekelezwa miradi hiyo kuitunza ili iendelee kuwa na manufaa kwao na taifa.

Killimbah aliziomba taasisi za Serikali kama Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka miundombinu kwenye miradi yote iliyotekelezwa lakini hakuna miundombinu hiyo ukizingatia kuwa miradi hiyo Serikali imetumia fedha nyingi kuikamilisha.

Aidha  Killimbah amewaomba waandishi wa habari kuandika habari za maendeleo  inayofanywa na Serikali katika halmashauri ili wananchi waweze kuielewa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anatoa fedha nyingi za miradi hiyo.

Pia  Killimbah aliziomba halmashauri zote za wilaya mkoani hapa kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili waweze kuandika habari hizo kwa nafasi kubwa kutokana na umuhimu wake katika jamii na nchi kwa ujumla.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo waliwapongeza viongozi wote wa wilaya hiyo, wakuu wa idara pamoja na wataalamu kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kufanikisha miradi hiyo kutekelezwa kwa uaminifu  na ufanisi mkubwa.

Baadhi ya  miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo upanuzi wa Mtandao na huduma ya Majisafi Singida mjini kupitia program ya IFF-OBA ambao gharama yake ni Sh.756,552,453.38 uliopo eneo la Somoku, Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Uhamaka unaotekelezwa kwa gharama ya  Sh.470,000,000 kupitia mradi wa SEQUIP 2021/2022.

Miradi mingine iliyokaguliwa ni ujenzi wa Kituo cha Afya Mandewa  kinachojengwa kwa fedha za tozo kutoka Serikali Kuu Sh.250,000,000, ujenzi wa Zahanati ya Ititi iliyogharimu Sh.50 Milioni na Ujenzi wa Jengo la Mionzi Kituo cha Afya Sokoine ambao umegharimu Sh.120,333,4000.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: