MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amefanya Mkutano wa hadhara katika Kata ya Ikungi ili kutoa mrejesho wa bajeti na miradi ya maendeleo kwa wananchi inayotekelezwa katika Jimbo hilo.

Aidha,amewahamisha wananchi kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na makazi Ili serikali iweze kupanga mipango yake kwa idadi ya watu waliopo

Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 5,2022,Ikungi Mjini,Mtaturu ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kupeleka fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Wakati awamu ya sita inakamilisha mwaka mmoja madarakani tunashuhudia miradi ikitekelezwa kwa kasi kubwa,tumepokea Sh Bilioni 2.6 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 67 ikiwemo shule ya Sekondari na shule shikizi na tayari yameshakamilika,"

Amesema kukamilika kwa madarasa hayo kutapunguza msongamano mashuleni na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea muda mrefu.

"Tumepokea fedha Sh Milion 800 ili kumalizia hospitali yetu ya wilaya,. sh Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Ntuntu na Sh Milioni 100 kujenga zahanati 2 za Makotea na Msule,"alisema.

Aidha amesema wamepokea Sh Bilioni 1.56 kwa ajili ya miradi ya maji vijiji vya Sakaa,Mukungu,Wakihendo, Minyinga, Matare na Ikungi mjini.

"Pamoja na haya serikali pia imekubali kujenga Kilometa 2 za lami Ikungi Mjini na kuweka taa za barabarani,haya ni maombi yangu ya muda mrefu ambapo niliomba kilomita 3 za lami mbele ya Waziri Mkuu alipofanya ziara Ikungi mwaka 2019,

"Kwa kipindi hiki Rais Samia anapotimiza mwaka mmoja tunasema mama ameupiga mwingi sana hadi kaondoka na magoli,"aliongeza.

Ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kushiriki zoezi la anuani ya makazi linalotekelezwa kwenye mitaa na vijiji.

"Mazoezi haya yana faida kwetu, Sensa ya watu na makazi itafanyika mwezi Agosti Mwaka huu na kupitia zoezi hili serikali itapata makadirio sahihi ya namna ya kuwahudumia wananchi,na tukumbuke fursa hii huja kila baada ya miaka 10 na mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2012 na sensa ya mwaka huu itakuwa sensa ya 8 toka sensa ya kwanza ya mwaka 1967,"aliongeza

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: