OR - TAMISEMI


Serikali yazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa zihakikishe zinafuata utaratibu uliopangwa katika utekelezaji wa Mardi wa DADPs.


 Kauli hiyo imetoewa wiki iliyopita Jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa wakati akiongea na wataalam wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Kilimo na Wadau kutoka Alliance for a Green Revolution in Africa-AGRA.


Waziri Bashungwa amesema, Mpango wa Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (DADPs) utasaidia kuongeza uzalishaji na kuongeza mapato lakini pia amesema kwa mwananchi utasaidia kuwa na malengo katika kufanya shughuli za uzalishaji wenye kuleta tija.  


Aidha,  uratibu wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa  “Strengthening Coordination of ASDP II at Local Government Authorities (SCALGA) Waziri Bashungwa amesema, ili kuwezesha Halmashuari zetu kuweza kufanya kazi za kilimo katika kuongeza uchumi wanchi na  kwamwananchi nazielekeza Mamlaka za Serekali za Mitaa kutotumia tofauti maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.


Pia nawaelekeza Maafisa Ugani ambao nyie ndio wataalam mlioko huko niwaelekeze msimamie kazi zenu na ukiwemo huu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo, huu mpango ni sekta ya uvuvi, kilimo na mifugo muhakikishe wananchi wetu wanafanya shughuli zao za uzalishaji na wananufaika nazo.


“Huu Mpango umetupa muongozo  watalaam, mradi huu ni wa awamu ya pili sasa nitoe wito kwa viongozi wenzangu ukianza kutekelezwa tukausimamie ili wananchi tunaoenda kuwasimamia wanakuwa na maslahi nao” amesisitiza Mhe. Bashungwa


Serikali inatambua  kila Halmashauri inampango  wake ila Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP) utaanza kutekelezwa katika Mikoa 12 na Halmashauri 30  Kagera (Muleba, Misenyi na Biharamulo), Kigoma (Kasulu, Kibondo na Kakonko), Katavi (Tanganyika, Mpimbwe na Nsimbo), Rukwa (Kalambo, Nkasi, Sumbawanga DC), Ruvuma (Songea DC, Madaba na Mbinga DC), Njombe (Wanging’mbe, Ludewa), Iringa (Mufindi, Kilolo), Manyara (Babati, Hanang na Kiteto), Arusha (Meru, Karatu na Arusha DC), Kilimanjaro (Hai, Siha na Rombo), Simiyu (Maswa) na Tanga (Kilindi). 


Mpango wa Mradi wa “District Agriculture Development Plan” (DADPs) ulizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa tarehe 3 Machi, 2022 Jijini Dodoma.

Share To:

Post A Comment: