Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb)ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa kuendeleza Bonde la Mto Songwe Mkutano unaofanyika Lilongwe Malawi.


Mkutano huo unaojumuisha nchi mbili za Tanzania na Malawi unajadili namna ya kukabiliana na mafuriko ya mto Songwe ambapo kwa Tanzania unapitiwa na Wilaya tano ambazo ni Mbozi,Mbeya Vijijini,Ileje,Kyela na Momba ambapo kwa Malawi unapitiwa na Wilaya za Karonga na Chitipa ambapo mto Songwe humwaga maji yake ziwa Nyasa.


Aidha mkutano unajadili namna ya kudhibiti kuhama hama kwa mto Songwe.


Share To:

Post A Comment: