Na Angela Msimbira MARA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuhakikisha Mameneja TARURA wa Mkoa yote nchini wanatoa Ripoti kila mwezi  kuhusu kazi zao kwa kuwa moja ya kigezo cha kuwapima ni utendaji kazi uliotukuka. 


Mhe. Bashungwa ametoa agizo hilo Leo kwenye uwekaji wa Jiwe la msingi kwenye  Mradi wa Majisafi wa Mugambo-Kiabakari-Butiama katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.


Amesema kazi ya Mameneja Mkoa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa  na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara zinasimamiwa kwa weledi na kuhakikisha thamani ya fedha ya fedha inaonekana kwenye ubora wa miundombinu ya barabara inayotekelezwa.


Mhe. Bashungwa amesema Ofisi ya Rais - TAMISEMI inaendelea kufanya maboresho  kwa Wakala  wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA)  ili iweze kusimamia kikamilifu  fedha zinazotolewa na Serikali katika ujenzi ya miundombinu ya barabara nchini ili kuwafungulia wananchi barabara za vijijini na  kufika kusikofikika.

Share To:

Post A Comment: