Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wameendelea kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwakomboa kupitia miradi inayotekelezwa na feha za tozo za miamala.


 Shukrani hizo zinafuatia baadaya kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Tarafa ya Sindeni chenye thamani ya Milioni 250 kwa fedha za tozo za miamala ya simu. 


"Tunamshukuru Mhe. Rais, Mama yetu Samia kwa kutuletea huduma hii ya Afya kwani tulikuwa tunateseka sana kwa kutembea umbali mrefu sana kwenda kutafuta huduma za Afya" walisema



Aidha Mkuu wa wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Handeni Saitoti Zelothe kusimamia kituo hicho kinaanza kutoa huduma haraka, kwa wananchi.


Miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini imetokana na fedha za tozo ambayo imewapunguzia adha ya utoaji wa michango wananchi na kuwapa fursa ya kuleta maendeleo ya familia kupitia fedha ambazo wangezitoa katika michango mbalimbali.

Share To:

Post A Comment: