Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha,Zelote Steven ameagiza hospitali ya wilaya ya karatu kuanza mara moja ili kusogeza huduma kwa wananchi kwa lengo na kutimiza malengo ya serikali yaliyokusudiwa.

Akizungumza katika kuelekea maadhimisho ya miaka 45 ya CCM ambapo mkoani Arusha yamefanyikia wilayani Karatu,Zelote alisema ni vyema hospitali hiyo ikaaza kutoa huduma kwa wananchi na kuachana na dhana ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

"Pamoja na hilo  hospitali ya wilaya ya karatu  ianze kazi kwa juhudi zote za kutoa huduma kwa wananchi na isingependeza kusubiri kiongozi wa nchi ndio aje atoe agizo,"alisema Mwenyekiti huyo

"Ndani ya mkoa wa Arusha serikali imefanikiwa kujenga madarasa zaidi ya 513 ya fedha za Uviko hivyo ni vyema wazazi wakaendelea kuwahimiza wanafunzi kwenda shuleni kusoma kwani wameondolewa adha ya michango ya ujenzi wa madarasa pamoja na ununuzi wa samani za shule,"alisema Zelote.

Vilevile alisema wakishirikiana kwa pamoja  watafanikiwa kutomeza   mauaji yanayojitokeza hivyo ni vyema  vyombo vya dola vikafanya kazi yao ili kulinda amani ya nchi ambayo ni tunu katika nchi ya Tanzania.


Naye Mkuu wa wilaya ya karatu, Dadi Kolimba alisema fedha za uviko kwa ajili ya ujenzi wa madarasa walipokea takribani sh.bilioni 1.2 kwa vyumba 60 ambapo umekamilika kwa asilimia 100 na wanafunzi wanaendelea na masomo.


Hata hivyo alisema hadi sasa wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza ni takribani watoto 3301 kati ya 4000 sawa na asilimia 74 hivyo aliwasisitiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule na kuanzia wiki ijayo watapita nyumba kwa nyumba kuhakikisha vijana hao waliobaki wanaenda shule.

"Haiwezekani serikali inaboresha mazingira ya shule alafu watoto hawapelekwi shule na wazazi wao tutapita nyumba kwa nyumba kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake,"alisema.


Alisema kwa upande wa ujenzi wa hospitali ya wilaya unaogharimu zaidi ya sh.bilioni mbili kupitia fedha za uviko upo katika hatua za mwisho za kukamilika ambapo majengo hayo ni  jengo la utawala,OPD, maabara na jengo la dawa.









 

Share To:

Post A Comment: