Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakiwasili katika viwanja vya Shule Shikizi ya Namba 7 iliyopo Kata ya Mang'onyi kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika juzi katika kata hiyo kiwilaya. kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM  wilaya hiyo, Mika Likapakapa, Mkuuu wa Wilaya Jerry Muro, Diwani wa Kata hiyo Innocent Makomelo na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Stanley Shabani.
Mwenyekiti wa CCM  wilaya hiyo, Mika Likapakapa akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkuuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga (kulia) akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Wengine wote ni madiwani wa wilaya hiyo.
Viongozi wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga, DC wa Ikungi Jerry Muro, Mwenyekiti wa CCM Mika Likapakapa, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mang'onyi Stanley Shabani na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendego.

Baadhi ya wataalamu wa wilaya hiyo wakishiriki maadhimisho hayo.

Wanafunzi wa Shule ya Shikizi Namba 7 wakiwa mbele ya madarasa waliojengewa na Kampuniya Uchimbaji Madini ya Shanta.

Sherehe zikiendelea.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye sherehe hizo.
Wanafunzi  na wazazi wao wakiwa kwenye sherehe hizo.

Taswira kwenye sherehe hizo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Abubakari Muna akitoa salamu katika maadhimisho hayo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Ally Rehani akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo.
Diwani wa Kata ya Mang;onyi, Innocent Makomelo akizungumza kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Viti Maalumu  Kata hiyo  Fatuma Makula akichangia jambo kwenye maadhimisho hayo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Shanta Mhandisi Kundael Ntiro akitoa taarifa ya miradi iliyotekelezwa na kampuni hiyo wilayani humo.
Burudani zikitolewa.
Viongozi na makada wa CCM wakiserebuka kwenye hafla hiyo.
Kadi zikitolewa kwa Wanachama waliojiunga CCM.
Kadi zikitolewa kwa Wanachama waliojiunga CCM.
Kadi za Chadema zikipokelewa na Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa baada ya kujiunga na chama hicho.
Kadi zikitolewa kwa Wanachama waliojiunga CCM.
Wanachama wapya wakila kiapo.
 


Na Dotto Mwaibale Singida


MKUU wa wilaya ya Ikungi Jerry Muro ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayeingia katika wilaya hiyo kwa nia ya kutaka kufanya uhalifu wa kutumia silaha kuwa hataweza kutoka salama kwa kuwa vyombo vya usalama vimejipanga ipasavyo kukabiliana na matukio yote ya kiharifu na kuwa wilala hiyo ipo  salama. 

DC Muro aliyasema hayo juzi wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyoazimishwa kiwilaya katika Kata ya Mang'onyi wilayani humo.

" Ndani ya miaka 45 vyombo vya ulinzi na usalama vimedumisha amani na ulinzi kwa kushirikiana na raia wema hatua iliyosababisha wilaya kuendelea kuwa salama na wananchi kuendelea na shughuli za maendeleo pasipo mashaka yoyote" alisema DC Muro.

Alisema mtu awaye yeyote asijaribu kuingia katika wilaya hiyo kwa nia hofu ni lazima atakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Mika Likapakapa alisema kuwa nchi yetu hususani Wilaya ya Ikungi imekuwa na mafanikio makubwa ya ujenzi wa barabara na miradi mingi  a hiyo yote imetokana na mfumo uliopo nfani ya chama hicho ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Aliutaja mfumo huo kuwa ni wa mafiga matatu akimaanisha Jumuiya ya Wazazi, Vijana na UWT na kuwa alifanya hivyo lengo likiwa kuwasogezea wananchi wapate huduma karibu.

Likapakapa alisema  mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa chama ambao kwa ngazi ya mashina utakuwa Aprili 10 hicho hivyo kila mwana chama anaruhusiwa kuchukua fomu na kugombea kwani hakuna mtu ambaye alizaliwa ili awe kiongozi  bali wote wanaweza kugombea na kuwa viongozi.

Diwani wa Kata ya Mang'onyi Innocent Makomelo alitumia maadhimisho hayo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kujenga miradi mbalimbali katika wilaya hiyo na kuwa kiu kubwa waliyokuwa nayo ni kujengewa madarasa katika Shule Shikizi ya Namba 7.

" Mwaka juzi wananchi wa kata hii waliomba mambo yote wayaache badala yake washughulikie suala la elimu kwanza na mimi niliyapokea kunapo husika na sasa tumepata madarasa" alisema Makomelo.

Makomelo aliomba shule hiyo isajiriwe na kupata walimu kutoka serikalini ili watoto hao wapate elimu iliyotarajiwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga aliishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelea fedha za kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema mwishoni mwa mwaka uliopita wilaya hiyo ilipokea zaidi ya Sh. Bilioni 2.6 kwa ajili ya miradi mbalimbali ambazo zilienda kutatua miundombinu ya ujenzi wa shule za sekondari, msingi na shikizi ambapo jumla ya madarasa 103 yamekamilishwa.

 Katika kilele cha maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zilizofanyika ni kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo barabara ya kilomita tatu, madarasa manne Shule Shikizi ya Namba 7, ujenzi wa vyoo na madarasa mawili shule ya Msingi Mlumbi, mradi wa maji utakao hudumia wananchi wa vijiji vya Mang'onyi na Mlumbi, ukarabati wa Zahanati ya Kata ya Mang'onyi pamoja na ujezi wa kichomea taka za uzio wake katika zahanati hiyo miradi hiyo yote imetekelezwa na Kampuni ya uchimbaji Madini ya Shanta kwa gharama ya Sh.235,495,327.

Shughuli nyingine iliyofanyika ni kuwapokea wanachama wapya wakiwemo viongozi 11 waliohamia CCM wakitokea upinzani sambamba na kukabidhi kadi zaidi ya 100 kwa wanachama wapya.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: