Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wameupongeza Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kwa kazi nzuri wanayoifanya hususani katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia Mfumo wa Force Account.


Akizungumza mara baada ya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi inayoendelea Chuoni hapa leo tarehe 17 February 2022; Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Omary Lumato amesema uongozi wa Chuo umeonesha moyo wa uzalendo katika utekelezaji wa miradi hiyo.


“Tunakupongeza Mkuu wa Chuo na menejimenti yako, tumetembelea miradi na tumeridhishwa na thamani ya fedha za Umma, uwazi, uzalendo na uwajibikaji; matumizi ya force account kwenye ujenzi wa miradi hii yamesaidia kuokoa fedha nyingi hongereni sana,” alisema Lumato.


Aidha, Lumato ametoa wito kwa Chuo cha Uhasibu Arusha kutoa elimu ya matumizi ya Force Account katika utekelezaji wa miradi kwa Taasisi nyingine za Umma, ili ziige mfumo huu na kuokoa fedha ambazo zinaweza kuelekezwa katika miradi mingine itakayowanufaisha wananchi.


Katika hatua nyingine Lumato amepongeza Chuo Cha Uhasibu Arusha kwa kuanzisha Kiotamizi ambacho kinawasaidia vijana kubuni na kutekeleza mawazo ya biashara ili kuwaandaa kujiajiri na kuwaajiri vijana wenzao, huku akihimiza vijana hao wahamasishwe kuomba mikopo ya vijana kutoka Halmashauri kukuza mitaji yao.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Cairo Mwaitete akieleza mafanikio ya Chuo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018/2019 hadi 2021/2022 amesema kumekuwa na ongezeko la udahili wa wanafunzi kutoka 3200 hadi 9890 na mitaala imeongezeka kutoka mtaala 17 mwaka 2018/2019 hadi mitaala 78 mwaka 2021/2022


Dkt. Mwaitete ameongeza kuwa Chuo cha Uhasibu Arusha kinakuwa kwa kasi, pamoja na kuwa na Kampasi ya Arusha, Babati, Dar es Salaam na Dodoma, Chuo kinatarajia kufungua Kampasi Mpya Mjini Songea ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi kama sehemu ya utekelezaji wa Sera za nchi.


Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia Force Account, Dkt. Mwaitete amesema Chuo cha Uhasibu Arusha wamefanikiwa kutekeleza kwa ufanisi kutokana uzalendo na uadilifu wa watumishi, hivyo akatoa wito kwa vijana kuwa waadilifu na wazalendo kwa nchi yao kwa maslahShare To:

Post A Comment: