Meneja Miradi wa TANCDA Happy Nchimbi (aliyesimama)akifurahia na washiriki wa mkutano huo

SHIRIKISHO la Vyama vya Magonjwa Yasioambukiza Tanzania (TANCDA) limesema limeridhishwa na majadiliano,moani ,ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwemo wabunge katika kuangalia nini kifanyike kushiriki magonjwa yasiyoambikiza ambayo yamekuwa tishio nchini.


TACDA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya iliona haja ya kuandaa mkutano na wadau hao kwa lengo la kuwasilishwa muhtarsari wa sera mbalimbali kuhusu lishe na ufanyaji mazoezi.

Akizungumza kuhusu mkutano huo Meneja Mirado wa TANCDA Happy. Nchimbi amesema wameridhishwa na washiriki wa mkutano huo kwani matarajio yao yamefikiwa kutokana na kupokea maoni na ushauri ambao watafanyia kazi.

"Ndicho tulichokuwa tunatarajia kikubwa ilikuwa nikuwasilisha muhtarsari wa sera mbalimbali juu ya lishe na ufanyaji mazoezi na yamepokelewa vizuri na maoni na ushauri yamekuwa mazuri ,hata waheshimiwa wabunge wamepokea na wameonesha watafanyia kazi.

"Lakini katika mkutano huu tulikuwa na Mkurugenzi wa Magonjwa Yasioambukiza kutoka Wizara ya Afya ambaye naye kwa pamoja kupitia sera ambazo zimewasilishwa juzi na jana ametoa agizo na ametoa mapendekezo ya kuanzisha kampeni ya pamoja ya kupambana na magonjwa yasiyoambikiza ambayo na sisi tunaahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha kwamba tunafanikisha hilo,"amesema Nchimbi.

Katika mkutano huo wadau Wengine walishiriki ni Chama cha 
wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) maofisa wa Wizara ya Afya
kupitia Mradi wa RECAP unaosimamiwa pia na shirika la afya Duniani, waandishi wa vyombo vya habari pamoja na mashirika na Taasisi za umma na binafsi.

Aidha katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro Antipas Mgungusi ... ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa TANCDA kwa kuwashirikisha waandishi kutoka vyombo na kwamba wakiwa sehemu ya majadiliano na kampeni zinazoendelea kuhusu kudhibiti magonjwa yasiyoambikiza itakuwa rahisi jamii ya Watanzania kupata taarifa sahihi kuhusu harakati hizo .

"Uwepo wa waandishi hapa ni muhimu sana, tunafahamu tutaweka mipango lakini ili wananchi wajue lazima waandishi wa habari watoe taarifa,katika mkutano huu wameshirikishwa ,hili ni jambo la kupongeza,"amesema Mgungusi huku akitoa rai pia kwa wanawake nchini kuwa mstari wa mbele katika kuzikinga familia dhidi ya magonjwa yasiyoambikiza kwa kuandaa mlo bora kwani magonjwa hayo yanatokana na mtindo mbaya wa maisha ikiwemo ulaji vyakula.

Mbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro Antipas Mgungusi akichangia wakati wa mkutano huo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Cecilia Daniel Parreso wa kwanza(kulia) akifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa uwasilishwaji wa sera kuhusu Magonjwa Yasioambukiza
Share To:

Post A Comment: