Julieth Ngarabali.  


Chuo kikuu cha Taifa cha Siasa ,Uongozi na maadili cha Mwalimu Nyerere ambacho kimejengwa  Kibaha Mkoani Pwani kwa ushirikiano wa vyama sita rafiki vilivyopigania  ukombozi katika nchi za kusini mwa Afrika kitazinduliwa rasmi februari 23 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Pwani Saidi Goha amesema uzinduzi huo utatanguliwa na ufunguzi wa barabara ya Muungano yenye urefu wa kilomita mbili uliyojengwa kwa kiwango cha lami ambao utafanywa Februari 22 na Katibu Mkuu CCM Taifa Daniel Chongolo.


Goha amesena hayo Februari 20 akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha na kuongeza kuwa vyama washirika vya ZANU -PF ya Zimbabwe, SWAPO ya Namibia , NBRA ya Angola , FLERIMO  ya Msumbiji na NPLL ya Angola zitashiriki kwenye uzinduzi huo.


"Rais wa Jamuhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa anakuja Kibaha Februari 23 asubuhi kuzindua chuo cheti hiki na vyama hivi washirika nao watashuhudia namna chama chetu kinavyotimiza majuku yake kwa hiyo kupitia wasaa huu nawaomba wananchi wa Pwani wajitokeze kwa wingi"amesema Goha.


Nao baadhi ya wakakazi wa Kibaha ilipo chuo hucho wameshukuru kujengwa katika eneo hilo kwa sababu wamepata fursa  ya kupata barabara ya kiwango cha lami ambayo imeondoa kero ya usafiri uliokuwepo awali kutokana na ubovu pamoja na kuongezeka mzunguko wa biashara zao ndogondogo ikiwemo mboga mboga


Chuo hicho cha Siasa ,Uongozi na Maadili cha Mwalimu Nyerere Kibaha Julai mwaka 2018 ndio kiliwekwa jiwe la msingi na Hayati Rais awamu ya tano Dr. John Magufuli  na kwamba kimejengwa kwa zaidi ya sh. Bil 100 na kitakua ni chuo cha masuala ya siasa,uongozi na maadili.

Share To:

Post A Comment: