Asila Twaha, OR- TAMISEMI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewataka Viongozi kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia kikamilifu matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi ili kusaidia upatikanaji wa huduma kirahisi kwa wananchi.


Mhe. Bashungwa amesema hayo leo Jijini Dodoma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Samia   Suluhu Hassan  kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu mfumo wa anwani za makazi  amesema, Ofisi ya Rais, TAMISEMI  imeshirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  kutoa  maelekezo kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa utekelezaji wa anwani za makazi.


Amesema kwa  majukumu yaliyotekelezwa na Wizara kwa kushirikiana na  wadau  kuhusu anunwani za makazi ni pamoja na kuandaa miongozo ya mfumo wa anwani za makazi, kutunga sheria ndogo, utambuzi wa majina ya mitaa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 Nchi nzima, kuandaa ramani za mipaka ya kiutawala, kujumuisha masuala ya mfumo wa anwani za makazi kwenye mwongozo wa mpango na bajeti katika mfumo wa undaaji wa bajeti.


Mhe. Bashungwa amemuhakikishia Mhe. Rais Samia  Ofisi ya Rais, TAMISEMI itaendelea   kuratibu na kusimamia anunwani za makazi zinatekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau ifikapo Mei,2022 kama ilivyoainishwa katika mpango husika na uandaaaji wa ramani msingi na kuanzia ngazi ya kitongoji, mtaa, kata  mpaka Mkoa.


 Amezielekeza Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinahakikisha zinashirikiana na wadau  kuandaa majina ya barabara na mitaa na kuziwasilisha Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.


“Ninazielekeza Sekretarieti  za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  kuhamasisha wananchi  na wadau washiriki katika usimakaji wa nguzo za majina  ya barabara na mitaa, kubandika vibao vyenye namba za nyumba  na mitaa” amesema Mhe. Bashungwa


Aidha, amesema utoaji wa elimu kwa viongozi, watendaji na wananchi kuhusu utekelezaji na matumizi ya mfumo wa anwani za makazi  unazingatiwa na  amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza maendeleo kwa wananchi.

Share To:

Post A Comment: