Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Balozi Ali Idi Siwa (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mhe. Partobas Katambi ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (katikati) wakati wa ziara ya kikazi waliyoifanya na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Joyce Ndalichako (hayupo pichani), ambapo walitembelea NSSF ikiwa ni moja wapo ya Taasisi iliyo chini ya Wizara hiyo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Balozi Ali Idi Siwa (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mhe. Profesa Joyce  Ndalichako, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (katikati) wakati wa ziara ya kikazi katika ofisi ya NSSF Makao makuu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NSSF, Dar es Saalam. Katika ziara hiyo alifuatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Partobas Katambi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NSSF, Dar es Saalam. Katika ziara hiyo alifuatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Partobas Katambi.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NSSF, Dar es Saalam. Katika ziara hiyo alifuatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Partobas Katambi.
 


Na Mwandishi Wetu


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuifikia sekta rasmi na sekta isiyo rasmi.

Aidha alifurahishiwa na namna uongozi wa Mfuko ulivyofanikiwa kuongeza idadi ya wanachama na kupelekea thamani ya Mfuko kuendelea kukuwa. 

Profesa Ndalichako alisema hayo jana katika ziara yake alipotembelea makao makao makuu ya NSSF jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara yake ya kwanza tokea alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.

Aliupongeza Mfuko kwa kupata mafanikio mbalimbali ambapo aliwaomba kuongeza juhudi za kufuatilia michango ya wanachama kwani kuna baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wana changamoto ya kutowasilisha michango ya wanachama wao kwa wakati.

Alisema kazi nzuri kubwa inayoendelea kufanywa na watumishi wa Mfuko inaleta matokeo chanya hasa katika kuongeza idadi ya wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi jambo ambalo linapelekea makusanya kuzidi kuongezeka.

Profesa Ndalichako alikiri kuwa ndani ya mwaka mmoja malalamiko ya wanachama wa NSSF yamepungua tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo baadhi ya wanachama walikuwa wanaomba msaada ili waweze kulipwa mafao yao.

“Ukweli ni kwamba sasa malalamiko mengi yamepungua na taarifa niliyopatiwa hali inakwenda vizuri…nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuwahudumia Watanzania na kuwapa elimu ya kujiwekea akiba kwa ajli ya maisha yao ya sasa na ya baadaye,” alisema.

Hata hivyo aliuomba uongozi wa NSSF kuweka mkazo katika sekta isiyo rasmi kwa sababu ni sekta ambayo inakuwa sana hivyo waendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali wakiwemo mama lishe, bodoboda, wavuvi, wakulima, wachimbaji wadogo wa madini pamoja na wajasiriamali wengine wote waweze kujiunga na NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzee.

Profesa Ndalichako alifurahishwa namna ambavyo Mfuko umejipanga kufikisha huduma zake kwa kutumia mifumo mbalimbali ya Tehama hatua ambayo itarahisisha zaidi upatikanaji wa huduma na kuwafikia wanachama wengi.

Kuhusu uwekezaji, Profesa Ndalichakao aliupongeza Mfuko kwa kufanya uwekezaji ambao ni moja ya jukumu lao la msingi na kwamba ameona miradi mingi wanayofanya ya uwekezaji na kuwataka miradi ambayo inachangamoto waendelee kuchukua hatua ili kuikwamua.

Awali, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Partobas Katambi alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mfuko huo yanatokana na kazi kubwa inayofanywa na watumishi wa NSSF hasa katika kutekeleza majukumu ya msingi.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, alimshukuru Waziri Ndalichako na kumuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Balozi Ali Iddi Siwa, alisema Mfuko uko katika mikono salama na kwamba tayari makusanyo ya michango yanaendelea kukuwa.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: