Na Prisca Libaga Maelezo/Arusha.


KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda, amehimiza kuimarishwa kwa utoaji wa elimu na uhamasishaji kwa wananchi katika ngazi zote za utawala wa nchi  ili washiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini Agosti mwaka huu.


 Amesema ili wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa ni muhimu kwa wadau wote, katika ngazi zote kuelewa umuhimu na manufaa ya sensa kwa ajili ya maendeleo yao na nchi yao.


 

“Sensa hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura ya 351 na umuhimu wake ni kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu, mahitaji yao na hivyo kuweza kupanga mipango ya maendeleo kwa uhakika zaidi.


 “Takwimu sahihi za kila mtanzania atakayehesabiwa siku ya sensa zitapatikana katika taarifa mbalimbali zitakazojazwa katika madodoso ya sensa hivyo kila mmoja wetu anapaswa kujitokeza ili ahesabiwe yakiwemo makundi maalum katika jamii,” amesisitiza

Share To:

Post A Comment: