Mbunge wa Jimbo la Kiteto  Edward Ole Lekaita amewataka viongozi wa dini na wananchi kuanza maombi  kuombea mvua kutokana na kuchelewa kunyesha hali inayosababisha mifugo kukosa chakula na mazao kunyauka shambani.


Ole Lekaita ametoa ombi hilo wakati akifanya mahojiano na kituo hiki ambapo amesema hali ya mifugo kwa sasa katika jimbo la Kiteto na mkoa wa Manyara kwa ujumla ni tete,mifugo haina nguvu.


Ameeleza kuwa Kipindi hiki ni kigumu kwa Wakulima na wafugaji kwa kuwa wengi wamezoea mvua zinanyesha kuanzia mwezi Novemba-Desemba lakini hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu ambapo hadi inafika katikati ya msimu mwezi Januari hakuna mvua.


Akitoa ushauri kwa wakulima, amesema katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mvua, wanatakiwa kulima mazao ambayo yanastahimili ukame.


Kwa upande mwingine amesema kwa sasa wanasubiri serikali kupitia wizara ya mifugo kutoa tathmini yakutosha kuhusu hali ya mifugo nchi nzima katika kipindi hiki.

Share To:

Post A Comment: