Joel Maduka Geita 

Mbunge wa jimbo la Msalala  Idd Kassim Idd  amekerwa na kusikitishwa na kitendo cha wakala wa barabara mjini na vijijini (  Tarura) halmshauri ya msalala Wilayani Kahama , Kwa kitendo  kuwapa tenda wazabuni wasio kidhi vigezo na kusababisha barabara kurudiwa pamoja na kutokukamilika kwa wakati 


Mbunge Idd  amesema hayo leo january 10, 2021 pindi alipokutana na maafisa wa Tarura katika kijiji cha Bubungu kata ya Jana ambapo amewata tarura wawe wanatoa taarifa za miradi inayotekelezwa ndani ya.  jimbo lake ili kuwaondolea hofu na kuwambia wananchi  namna serikali yao inavyopambana kuwarekebishia miundo mbinu kijiji kwa kijiji ,kata kwa kata nchi  nzima .


" Tarura mnasema mmepokea fedha za tozo  kwa ajili  ya  barabara lakini  amtoi  taarifa kwenye ofisi yangu Kama msimamizi wa Jimbo ni lazima mimi nijue mnatekeleza barabara gani , gharama gani ,na fedha kutoka wapi ili tuwaeleze wananchi sio mpaka tufumaniane site" 

Mbunge Idd  amechangia kiasi cha shillingi million 2.   ili kukamilisha ujenzi wa msingi wa  hosteli ya  shule ya Sekondari ya Kata ya  jana itakayowasaidia wanafunzi kukaa na kupata muda mwingi wa kujisomea sambamba na  kuepukana  na vishawishi vibaya vitakavyoharibu ndoto zao.

Share To:

Post A Comment: