Emanuel Msumba,Karatu

Mbunge wa Jimbo la Karatu Daniel Awack amewasilisha taarifa ya utekelezaji  wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha  mwaka mmoja tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ambapo miradi mbali mbali ya maji,umeme,miradi ya Covid 19 ya ujenzi wa madarasa  imetekelezwa katika jimbo hilo.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Karatu,Wanachama wa CCM pamoja na Viongozi wa Serikali ,Mbunge Daniel Awack amesemakuwa Jimbo hilo lilipokea fedha za kuchochea maendeleo ya jimbo milioni 54 ambazo zilielekezwa kwenye miradi ya elimu na afya.

Aidha kwa kipindi cha mwaka  cha mwaka mmoja serikali imetoa fedha za kutekelezamiradi ya maji kwa AUWSA na RUWASA kiasi cha Shilingi Bilioni 1 ambazo zimeelekezwa kwenye miradi ya maji ya AYALLABE na vitongoji sita vya Bwawani na Karatu Mjini.

Daniel ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za UVICO 19 kwa  wilaya ya Karatu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.9 ambapo imewezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 60.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: