Katibu Mkuu Mifugo Bw.Tixon Nzunda kulia akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka
kwa Mtendaji Mkuu TVLA Dkt.Stella Bitanyi kushoto juu ya ubora wa chanjo
zinazozalishwa na Taasisi yake. |
Na Kumbuka Ndatta
Katibu
Mkuu Mifugo Bw.Tixon Nzunda ameelekeza kwamba wakala wa Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) ifanye kazi Kibiashara ili iweze kujiendesha
yenyewe bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.
Hayo
ameyasema leo tarehe 26/01/2022 alipofanya ziara yake ya kwanza tangu
alipoteuliwa tarehe 08 Januari 2022, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Mifugo)
"Fanyeni
kazi kibiashara na kwa uadilifu mkubwa ,mashamba hayo yanayovamiwa na
Wananchi hakikisheni mnayatumia kibiashara, tengeni fedha kwenye bajeti
yenu ili yaweze kupimwa ili kuondokana na adhaa ya kuvamiwa na wanachi".
Alisema Nzunda.
Katika
ziara hiyo, Katibu Mkuu Mifugo Bw.Tixon Nzunda, ameelekeza, Mifumo ya
utendaji kazi ya Kielekroniki iimarishwe katika vituo vyote vya Wakala.
Pia,
katika kutatua changamoto ya Uhaba wa Watumishi wa wakala hiyo, katibu
Mkuu Mifugo amemweelekeza Mtendaji mkuu wa Wakala hiyo kufuatilia
maombi ya kuajiri watumishi wapya Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma ili
kukidhi mahitaji ya taasisi hiyo.
Vile
vile Nzunda ameelekeza kuwa Mali za wakala zilindwe, zitunzwe ili
ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Pia, ameelekeza Wakala
kufanya kazi kwa karibu na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) cha
Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kutangaza kazi nzuri zinazofanywa na
wakala hiyo.
Aidha,
Katibu Mkuu Mifugo ameielekeza Wakala hiyo kuandaa mkutano mmoja kila
mwaka ili kukutana na wadau wanaotumia chanjo hizo ili kupata mrejesho
kutoka wadau hao. Pamoja na Mambo mengine,Katibu Mkuu Mifugo ameelekeza
wakala wajikite katika kutafuta masoko ya chanjo hizo nje na ndani ya
nchi.
Awali Dkt.Stella
Bitanyi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa maabara ya Veterinari Tanzania
(TVLA) alitoa taarifa ya utendaji kazi wa (TVLA) kwa Katibu Mkuu Mifugo
Bw.Tixon Nzunda, kuwa, kazi kubwa wanayofanya ni pamoja na uchunguzi
na Utambuzi wa Magonjwa ya Wanyama na Wadudu wanaosambaza magojwa na
uhakiki wa usalama na Ubora wa Vyakula vya Mifugo.
Pia,
wakala inatimiza Majukumu yake kwa kupima,kutathimini na kuhakiki
Vitendanishi, mimea tiba pamoja na kemikali zinazotumika katika maabara
za Wanyama.Vile vile taasisi hiyo inafanya tafiti za Magonjwa ya wanyama
na Wadudu wanaosambaza Magonjwa hayo na kutoa Ushauri/teknolojia ya
kudhibiti Magonjwa husika na Wadudu waenezao magonjwa hayo.
Pia,
Dkt. Bitanyi amemwambia Bw. Nzunda kuwa TVLA inatengeneza na kuzalisha
aina saba (7) chanjo dhidi ya magonjwa ya Mifugo ikiwa ni pamoja
vitendanisha.
Aidha,
Chanjo za Mifugo zinazozalishwa na TVLA ni pamoja naTemevac,(chanjo
dhidi ya Mdondo), Kimeta, Chambavu,Tecoblax (Mchanganyiko wa Kimeta na
Chambavu), Kutupa Mimba (Brucellosis), Homa ya Mapafu ya ng'ombe (CBPP)
na Homa ya Mapafu ya Mbuzi (CCPP).
Dkt.
Bitanyi amesema kuwa ili kusogeza huduma karibu kwa wafugaji, vituo
hivyo vya uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo vipo pia katika mikoa ya
Arusha, Dodoma, Iringa, Mtwara, Mwanza, Sumbawanga, Tabora na Kliniki ya
Mifugo na Maabara meatu-Simiyu.
Vile
Vile Mtendaji Mkuu wa TVLA, amesema kuwa taasisi yake inakumbana na
changamoto kadhaa, baadhi ni pamoja na Uvamizi wa wananchi katika
mashamba yanayomilikiwa na wakala hiyo, inayotoka na kupanuka kwa Miji
na kutopatikana kwa hati miliki kwa baadhi ya Maeneo. Pia Mwamko mdogo
wa matumizi ya Chanjo na Huduma za Maabara.
Aidha,
Changamoto nyingine ametaja kuwa mtaji mdogo usioweza kuruhusu
Uwekezaji Mkubwa katika Kiwanda cha Uzalishaji chanjo hasa katika
kununua Mitambo na Mashine za kisasa kwa ajili kuzalisha chanjo.
Katibu
Mkuu mifugo, pia alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha
Chanjo kibaha (TVI) na kujionea jinsi chanjo za mifugo
zinavyotengenezwa.
Pia,
Nzunda aliipongeza taasisi ya TVLA kwa kazi nzuri wanayofanya na
kuwataka wanasayansi hao kuongeza umahili na Weledi katika kazi zao na
kuzingatia Uadilifu.
Post A Comment: