Picha mbali mbali za zoezi la uhamasishaji chanjo ya Uviko 19 awamu ya pili kwa mkoa wa Tanga katika vituo mbalimbali likiendelea kama walivyokutwa na kamera ya matukio katika wilaya za Kilindi Lushoto na Handeni picha zote kwa mwandishi wetu wa msumba news. Idadi ya wananchi imezidi kuongezeka tangia kuanza kwa uhamasishaji wa kupata chanjo ya Uviko 19 mkoani Tanga. Zoezi hilo liloanza Baada ya waziri wa Afya. Doroth Gwajima kulizindua mkoani Arusha limeonekana kushika kasi kwa wananchi kujitokeza kuchanjwa chanjo hiyo ya kujikinga na Uviko 19 Msumba news Imeshuhudia maeneo mbalimbali zoezi hilo likipita mitaani hukowananchi wakijitokeza kupata chanjo ya uviko 19 katika maeneo ya vijiji vya Mazinde Ng'waru na Msata. Akiongea mara baada ya ukaguzi wa vituo wilayani Handeni Mratibu wa timu ya uhamasishaji chanjoya Uviko 19 kitaifa kwamkoa wa Tanga Regina Richard amesema kuwa chanjo hiyo iende sambamba na afua zingine za udhibiti wa ungonjwa wa Korona Amesema sehemu ambazo Afua za ugonjwa huo hazijapewa kipaumbele zinatakiwa kuhakikisha zinaweka au kuboresha ilikuendanana vita hiyo ya Uviko 19
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: