Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi( Mb)amewata wazazi kuwalea watoto katika maadili ili waweze kufikia ndoto zao.


Mahundi ameyasema hayo katika hafla ya Frola Mnyandavila deareva wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya.


"Wazazi wengi wamekuwa wakikwepa majukumu ya malezi kwa kuwaachia walezi ambao baadhi huwafanyia ukatili pindi wawapo kazini vikiwemo vya ulawiti na ubaki"alisema Mahundi.


Alisema Frola ametoa somo kwa jamii kwa kutokata tamaa pindi wanapokutana na changamoto bali wazitumie changamoto kama fursa.


Kupitia changamoto alizopitia Frola ameamua kumsomesha mtoto mwenye ulemavu anayesoma shule ya Hayanga kwa mahitaji yote sambamba na kumpatia baiskeli mwendo kama sehemu yake ya shukurani.


Frola amepitia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya udereva ambayo yamemwezesha kujikimu kimaisha na kumudu kuwasomesha watoto.

Share To:

Post A Comment: