Nteghenjwa Hosseah, Tabora


Takribani Bili 1.48 za Mradi wa Maendeleo kwa Ustawi zimetolewa Manispaa ya Tabora kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 60 kwa ajili ya shule za Sekondari na madarasa 14  ya Vituo shikizi pamoja na Ofisi 34 za Walimu.


Taarifa njema ni kuwa ujenzi wa vyumba hivyo madarasa umekamilika kwa asilimia 100 na wanafunzi wote Waliofaulu wataanza masomo kwa awamu moja.


Akiwa ziarani katika Manispaa hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na kasi ya ujenzi na ubora wa miundombinu ya madarasa Mkoani humo.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani akitoa tathmini ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Mkoani humo amesema katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Halmashauri za  Tabora Manisapa na Nzega Tc wamekamilisha kwa asilimia 100 na halmashauri za Uyui, Urambo,Kaliua na Sikonge wakl kwenye asilimia 90 na kwa muda ulioongewa wa tarehe 31 Disemba,2021 watakua wamekamilisha kwa asilimia 100.


Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Peter Maiga Nyanya amesema wanafunzi waliomaliza kidato cha nne,2021 ni 2,579 na wanaotegemewa kuanza

Kidato cha kwanza 2022 ni 4,922 hivyo kwa madarasa haya 60 yaliyojengwa kwa awamu moja  wanafunzi wote wataanza kidato cha kwanza wataingia darasa siku moja.

Share To:

Post A Comment: