Naibu waziri wa maji mhandisi Marryprisca Mahundi ambaye pia ni mjumbe wa baraza la umoja wa wanawake mkoa wa Mbeya UWT amewashauri  wajumbe wa baraza hilo  kushirikiana katika kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa nyumba za makatibu wa umoja wa wanawake ili kufanikisha  malengo  ya UWT  taifa.


Naibu waziri wa maji mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa ushauri huo baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT mkoa wa Mbeya ambao mpaka sasa umegharimu zaidi ya shilling millioni Tano  na umefikia hatua ya msingi ambapo amewataka UWT kushikamana katika utelezaji wa miradi endelevu ikiwemo ujenzi wa nyumba  za makatibu.


 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mbeya Kibona amepongeza jitihada za naibu waziri wa wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi katika utekelezaji wa majukumu na ahadi zake  huku katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya.


Amesema ujenzi wa nyumba hizo tayari umeanza katika wilaya zote ikiwemo ya katibu mkoa ambayo ipo katika hatua ya msingi na imegharimu zaidi ya million 5.


Mjumbe wa baraza la umoja wa wanawake  mji mdogo wa makongolosi wilaya ya Chunya Pili Hussen amempongeza naibu waziri wa maji kwa kuwatia moyo katika kuhakikisha wanafikia hatua ya ukamilishaji wa jengo la nyumba ya katibu wa wilaya.

Share To:

Post A Comment: