Nteghenjwa Hosseah,Tabora


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Ummy Mwalimu amekagua miradi ya Elimu na Afya inayotekelezwa kutokana na fedha za tozo za miamala ya simu.


Akiwa katika Kituo cha Afya Ilolangulu kilichopo Tarafa ya Ilolangulu wilayani Uyui, Waziri Ummy ameridhishwa na kasi ya ujenzi kituo hicho na kusisitiza kazi hiyo ikamilike kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma.


"Mtakumbuka kuwa, tulitoa fedha za tozo kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 220 na hiki cha Ilolangulu ni miongoni mwa vituo vilivyopokea fedha za yozo, ninafurahi kuona fedha zetu wenyewe zimeweza kujenga kituo hiki ambacho kitatoa huduma kwa wananchi wa Tarafa hii ya Ilolangulu.


"Tuliposema fedha za tozo ya mawasiliano tunapeleka kwenye tarafa ambazo hazikuwa na kituo cha afya nadhani mmeona dhahiri kuwa hapa Ilolangulu hapakuwa na Kituo cha Afya na ni Tarafa kubwa iliyostahili kabisa kupata fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya,"amefafanua Waziri.


Wakati huo huo, Mhe. Ummy alitembelea Shule ya Sekondari Kigwa na kukagua ujenzi wa miundombinu ya darasa lililokamilishwa kwa fedha za tozo ya miamala ya mawasiliano.


Ujenzi wa darasa hilo ulianzishwa kwa nguvu za wananchi na waliletewa shilingi miliono 12.5 kutoka katika tozo ya miamala ya simu kwa ajili ya ukamilishaji.


Halkadhalika Katika shule hiyo ya Sekondari Kigwa  Mhe. Ummy amekagua ujenzi wa miundombinu ya ujenzi wa madarasa 6 yaliyojengwa kwa fedha za Mpango wa Maendeleo Kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 na haya ni kati ya madarasa 178 yanayojengwa katoka Wilaua ya Uyui.


Kati ya madarasa hayo 123 ni shule za Sekondari na madarasa 55  yanajengwa kwenye vituo shikizi.

Share To:

Post A Comment: