Na Rhoda Simba,Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka ameuagiza uongozi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji na Afisa Elimu kuhakikisha wanasambaza walimu wa sekondari katika shule zenye uhaba badala ya kuacha walimu kurundikana shule moja.
Aidha amesema zipo shule za sekondari ndani ya jiji ambazo zina walimu wengi na zilizopo pembezoni mwa jiji zina walimu wachache, kutokana na hali hiyo Ofisi ya afisa elimu na Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji waone namna ya kuweza kuwasambaza walimu waliokuwa wengi katika shule za pembezoni ambazo zina uhaba.
Mtaka ameyasema hayo leo Disemba 22 jijini hapa wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari zilizojengwa kwa fedha za mkopo wa mashart nafuu unaotokana na mapambano dhidi ya uviko 19.
Amesema Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa ambayo imefanikiwa kufanya ujenzi wa vyumba bora vya madarasa ambayo yana ubora wa kiwango cha juu
"Dodoma tumeweza kujenga madarasa yenye ubora unaoendana na thamani ya fedha lakini napenda kutoa maagizo katika Ofisi ya Mkurugenzi na afisa elimu kukutana mkaona ni namna gani ya kufanya utaratibu wa kupunguza
walimu waliozidi katika baadhi ya shule na kuwapeleka katika shule ambazo zina uhaba wa walimu,
"Na jambo hili liwekwe wazi kwa walimu kuwa ni kwa nia njema ili kuifanya elimu ya wanafunzi wa jiji la Dodoma kuwa bora zaidi na ilingane na viwango vya ubora wa madarasa" amesema Mtaka
Hata hivyo ametoa maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma na Ofisi ya afisa elimu wa jiji kutoa taarifa kwa wakuu wote wa shule kuwa pindi shule zitakapofunguliwa tarehe 17 January 2022 kila mwanafunzi awajibike kupanda miti na kuuutunza.
Nae Mkurugenzi wa jiji Joseph Mafuru amesema ujenzi huo unatarajia kabla ya sikukuu ya chris mass utakuwa umekamilka na funguo zitakabidhiwa tayari kwaajili ya maandalizi ya wanafunzi kuanza masomo.
Post A Comment: