Mti mkubwa wa maajabu ulioota katikati ya barabara wenye tundu kubwa wenye uwezo wa kupitisha magari watu na vyombo vya moto katika hifadhi ya Arusha National Park
Mkuu wa hifadhi ya Arusha National Park Kamishina msaidizi wa uhifadhi Albert Mziray akiongea na waandishi wa habari waliofika hifadhini hapo hivi karibuni
Hapa ni Serengeti ndogo ukiwa katika sehemu hii utaweza kuona wanyama  kiurahisi

Basi la abiria likiwa linapita katika hifadhi ya Arusha National Park
Mhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi  la Taifa Tanapa Mohammed Kiganja azungumzia mti huo wa maajabu.


Na Pamela Mollel,Arusha

Maajabu ya mti mkubwa aina ya mkuyu ulioota katikati ya barabara wenye tundu kubwa wenye uwezo wa kupitisha magari,watu na vyombo vingine vya moto imekuwa kivutio kikubwa katika hifadhi ya Arusha national Park

Mti huo umevutia sana watalii wa ndani na nje ya nchi wanaofika katika eneo hilo kwa shughuli za utalii

Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya ANAPA Kamishina msaidizi wa uhifadhi Albert Mziray anasema mti huo ulikuwepo toka 1960 kutokana na umuhimu wake katika hifadhi watahakikisha wanautangaza zaidi ujulikane ndani na nje ya nchi

"Kitu cha kipekee katika hifadhi hii ni mti mkubwa ulioota katikati ya barabara wenye tundu kubwa katikati umekuwa kivutio kikubwa hapa hifadhini"alisema Mziray

Alisema Hifadhi hiyo itaendelea kuutangaza mti huo kama sehemu ya utalii unaopatikana katika hifadhi hiyo tu

Mbali na mti huo wa maajabu ukiwa katika hifadhi utaweza kuona Serengeti ndogo na sehemu hii utapata fursa ya kuona wanyama mbalimbali kwa ukaribu

Mhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanapa Mohammed Kiganja anasema mti huo ni wa kipekee sana hivyo wapenda utalii wajitokeze kwa wingi kujionea mti wa maajabu

"Yawezekana huu mti unapatikana katika hifadhi hii tu kwanza unavutia kwa muonekano "alisema Kiganja

Hifadhi ya Arusha national Park ilianzishwa mwaka 1960
Share To:

Post A Comment: