Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Mahawanga Janeth leo amekutana na Kamati ya Ujenzi na Uongozi wa Jumuiya ya Wanawake Wilaya ya Kigamboni na kukabidhi  tani tano za saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Kigamboni unaoendelea.


Mh. Mahawanga amefurahishwa na hatua nzuri inayofanywa na Kamati hiyo pamoja na uongozi mzima wa UWT Wilaya kwa kusimamia vyema zoezi hilo la  ujenzi wa nyumba hizo za Watumishi unaoendelea katika Wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa tani tano kwa kila wilaya ambapo alikwisha kabidhi katika Wilaya ya Temeke na Kinondoni na leo amekabidhi Kigamboni.


Aidha Mh. Mahawanga amesisitiza kuendelea kushirikiana nao kwenye kila hatua za ujenzi huo ili kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika kwa wakati lakini pia kuendelea kuungana pamoja kama Jumuiya kutekeleza jukumu hilo la ujenzi.


Mh. Mahawanga ametumia muda huo kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka mpya ujao wa 2022 sambamba na kuwashukuru kwa kipindi chote ambacho wameshirikiana katika mwaka huu 2021 unaokwenda kuisha na kuahidi kuendelea kushirikiana nao pamoja kwa vipindi vinavyokuja mwakani kuhakikisha Jumuiya ya Wanawake ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam inazidi kuwa imara sambamba na wanafikia lengo kubwa la kumkwamua Mwanamke kiuchumi.


Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigamboni amempongeza Mh. Mahawanga kwa utekelezaji wa ahadi yake mapema na kumhakikishia kamati itasimamia vyema ujenzi huo na watazidi kushirikiana kama timu ili kuhakikisha lengo linatimi. 

Pia amempongeza sana kwa kazi nzuri anayofanya ya kuhakikisha fursa za kuwainua Wanawake zinazidi kuwafikia Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam sambamba na kutoa Elimu kuhusiana na vikundi, kuwakutanisha na Wadau mbalimbali ili kuweza kufikia lengo kuu la kuwainua na kuwakwamua wanawake kiuchumi.



Share To:

Post A Comment: