Nteghenjwa Hosseah, Tabora


Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imetekeleza kwa vitendo Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwankutoka mkopo mkubwa utakaoleta tija kwenye vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.


Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake Mkoani Tabora wakati akikagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.


Akiwa katika Manispaa hiyo alitembelea Kiwanda cha Kuchakata Asali cha Miombo Neekiping Initiatives  kilichopewa Mkopo wa shilingi Milioni 50 zilizowezesha kuanzisha kiwanda ambacho kimetoa soko la uhakika kwa wafugaji takribani 178.


Akiwa katika Kiwanda hapo Waziri Ummy amewapongeza vijana hao kwa kuanzisha kiwanda kinachoongeza thamani ya Asali ambayo imewaongezea kipato na pia imesaidia kutoka fursa ya soko la uhakika kwa wafugaji 178.


“Sasa nyie muwe vijana wa mfano kwa kuhakikisha kuwa mkopo huu mliopewa ambao hauna riba  mnarejesha kwa wakati ili wengine nao waweze kufaidia;


Pia aliwataka  kutafuta eneo kubwa nje ya Mji ili waweze kujenga Kiwanda kikubwa kwa eneo wilopo sasa ni dogo” Alisema Mhe. Ummy


“Niwapongeza Manispaa ya Tabora kwa kutekeleza Agizo hili la Mhe. Rais na kuweza kutoa Mkopo mkubwa kwa kikundi hiki ambao bila shaka Tija ya Mkopo huu tumeshaanza kuiona na sio kama maeneo mengine wanatoa fedha kidogo ambazo hazileti matokeo’ alisisitiza Mhe. Ummy

Share To:

Post A Comment: