Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kwa Utashi wake wa kukusudia kuigawanya Wizara ya Afya amesema kuwa kutokana maagizo ya mkutano wa June 8 2021 jijini Dodoma.

Wizara zinazoshughulikia maswala ya Jinsia upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ilianza kulifanyia kazi agizo kwa kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza ahadi yake ya kuwa  kinara katika eneo la haki na usawa wa kiuchumi nchini ambapo wanawake na wanaume watakuwa na fursa na haki sawa katika kunufaika na uwezeshaji kiuchumi. 

Pamoja na kuzindua kamati hii leo,  Wizara  pia imeweza kuratibu uandaliwaji wa Mpangokazi Jumuishi na Shirikishi  wa Taifa.

Share To:

Post A Comment: