Katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro imeshiriki katika zoezi maalum endelevu kwa  kuotesha miti 8,000 katika maeneo ya Samanga na Singa wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.


Awali maeneo hayo  yalikuwa yameathiriwa na mimea vamizi jamii ya Miwato (Acacia Mearnsii) ambapo Hifadhi iliondoa mimea hiyo mwaka jana wa fedha. 


Mgeni Rasmi katika shughuli hii alikuwa Balozi wa Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Sharon Ringo. Wadau wengine walioshiriki ni wananchi wa Kijiji cha Samanga, wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya- Rombo na Maafisa kutoka Sekretariet ya Mkoa wa Kilimanjaro.


Pascal Shelutete

SAC CC

TANAPA
Share To:

Post A Comment: