Nteghenjwa Hosseah, Tabora


Kati ya vitu vinavyoniumiza kichwa ni kuona wimbi la watumishi wakitaka kuhama kutoka vijijini kwenda Mjini.


Nitakua Waziri wa hovyo kama nitaendelea kuruhusu uhamisho wa aina hii kwa sababu na kule vijini kuna watoto ambao wanahitaji walimu wa kuwafundishi na wananchi wanaohitaji wataalamu wa Afya wa kuwahudumia.


Ndoa haziko Mjini tu hata wa vijijini wameoa na kuolewa sasa kwanini kila mtumishi anayemfuata mwenza anakua kuhamia mjini ina maana hakuna wenza walioko halmashauri za pembezoni?


Haya ni maneno ya mara kadhaa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu anapokua kwenye ziara za kikazi katika mamlaka za Serikali za Mitaa na kuulizwa maswali kuhusu kusitisha kwa muda uhamisho wa watumishi.


“Nimefikiria mara nyingi namna gani naweza kuwamotivate watumishi wa Halmashauri za Vijijini ili waweze kufurahia mazingira yao ya kazi na kuacha kufikiria masuala ya kuhama na kwenda mjini” 


Kati ya vitu vya mwanzo nlivyopanga ni kujenga nyumba za watumishi hao ili waweze kuishi kwenye mazingira bora yatakayowavutia kufanya kazi katika maeneo ya vijijini.


Akiwa ziarani Mkoani Tabora katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui  mapema leo amesema  kuna wakati mtu anapangiwa kazi kijijini kiasi kwamba hata nyumba ya kupanga ya maana hakuna lakini tukijenga nyumba nzuri eneo hilo ntumisni huyo atakua na uhakika wa makazi bora.


Katika kutekeleza hilo tumepata shilingi bilioni 6 kutoka katika ushuru wa huduma ya Mawasiliano na tumeelekeza fedha hizi zikajenga nyumba za watumishi 165 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Akielezea Nyumba hizo Waziri Ummy amesma zitakua nyumba 54 za 3 in 1; Yaan nyumba 1 itabeba familia 3 hivyo jumla itakua familia 162.


Amebainisha kuwa nyumba hizo zitajengwa kwenye Halmashauri za Wilaya na baadhi ya halmashauri za Mji ambazo hazina mapato makubwa; Halmashauri za Majiji na Mansispaa hazitapata fedha hizi kwa kuwa wanaweza kutumia mapato ya ndani kujenga nyumba za watumishi.Share To:

Post A Comment: