Shirika lisilo la kiserikali ECLAT FOUNDATION linalojishughulisha  na Maendeleo ya jamii katika nyanja mbalimbali kwa kushirikiana na shirika la UPENDO ASSOCIATION limeandaa mradi maalum wa kujenga shule ya msingi Idonyonado kwa madarasa nne itakayogharimu zaidi ya shilingi Millioni 300.


Mkurugenzi wa Shirika hilo Mhe Peter Toima aliyeongozana na Dr Fred Heimbach wa Shirika la  Upendo Association la Ujerumani amesema shirika hilo limekuwa likiwasaidia jamii nyingi nchini zilizopo nje ya miji na ndani ya miji katika Nyanja ya Elimu, Afya, Maswala ya wanawake na Maendeleo kwa ujumla, na kusema kwa mwaka Huu kupitia ofisi ya Mbunge Wa jimbo la Monduli wananchi wa kijiji cha Idonyonado Kata ya Mfereji watapata neema hiyo ya kujengewa shule ya msingi.


Hili limejiri katika ziara ya Mbunge wa jimbo la Monduli Fredrick Lowasa katika sehemu mbalimbali za jimbo hilo ambapo amesema kati ya Ahadi alizowahidi wananchi wa kijiji cha Idonyonado ni pamoja NA Elimu na Hili kwa leo linakamilika kupitia ufadhili wa ECLAT FOUNDATION NA UPENDO ASSOCIATION kupitia mradi wa ujenzi wa Madarasa manne kwa mujibu wa mkurugenzi, na kuahidi kutoa ushirikiano kwa namna yoyote ili kufanikisha Mradi.


Kwa upande wa wananchi wa kijiji hicho wamesema hiyo ni Neema kubwa kwao na kwa watoto wao na hili ninkutokana na jitahada zao kuanza kujenga shule kwa darasa moja , na sasa shule hiyo ina wanafunzi zaidi mia moja (100) na kuna ambao wamehamishwa shule ya msingi mfereji ambayo ni ya bweni na kwa sasa shule hiyo ina miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.


Shirika la ECLAT FOUNDATION lenye makao yake EMBOREET SIMANJIRO MKOANI MANYARA na UPENDO ASSOCIATION Lenye makao yake UJERUMANI inatarajia kuanza mradi huo mwanzoni mwa mwezi DECEMBER Mwaka huu.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: