Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa kumi na tatu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi URA SACCOS,uliofanyika jijini Mbeya.


Wajumbe mbalimbali wa wakifuatilia majadiliano wakati wa Mkutano Mkuu wa kumi na tatu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi URA SACCOS,uliofanyika jijini Mbeya.


Mrajis wa Vyama vya Ushirika (katikati) Dkt. Benson Ndiege akiwa na viongozi Pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa kumi na tatu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi URA SACCOS,uliofanyika jijini Mbeya.

....................................................................................................

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amevitaka vyama vya Ushirika kuongeza matumizi ya TEHAMA ili kufanya kazi kwa ufanisi na tija ya utekelezaji wa majukumu ya vyama pamoja na huduma bora kwa wanachama wa Ushirika.

Mrajis ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa kumi na tatu wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi URA SACCOS, Ijumaa Oktoba 29, 2021 mkoani Mbeya.

Akiongea katika Mkutano huo Mrajis amesema matumizi ya TEHEMA kwa vyama vya Ushirika yatasaidia watendaji kufanya majukumu yao kwa ufanisi kutokana na uwezo mzuri wa utunzaji sahihi wa kumbukumbu, utekelezaji wa majukumu kwa haraka, kuwafikia wanachama walio maeneo ya mbali. Amesema kufanya hivyo, wanachama watanufaika kwa huduma bora ambayo itasaidia kupunguza na hata kuondokana na migogoro isiyo ya lazima kwenye vyama vya Ushirika.

“Kwenye dunia ya sasa huwezi kukwepa TEHAMA kwahiyo nitoe wito kwa Vyama vyote vya Ushirika kutumia TEHAMA ili kutunza vyema takwimu za vyama na kuongeza usalama wa taarifa zetu vizuri,” alisisitiza Mrajis

Aidha, Mrajis amesisistiza vyama vya Ushirika kuzingatia taratibu za kufanya mikutano mikuu ya Chama kutokana na umuhimu wake katika kuhakikisha wanachama wanapata fursa ya kujua maendeleo ya Chama, kutoa mawazo ya kuendeleza vyama vyao. Hivyo, amewataka wanachama kutimiza wajibu wao wa ushiriki na kufuatilia mikutano mikuu ya vyama vyao vya Ushirika kwa kadri ya ratiba za Vyama.

Akiongelea URA SACCOS Dkt. Ndiege amekipongeza chama hicho kwa kupata Hati safi ya Ukaguzi kutoka kwa Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) akieleza kuwa hiyo ni hatua nzuri inayoonyesha uwajibikaji na nidhamu ya Chama. Hivyo, amewataka wajumbe wa Bodi pamoja na Watendaji kuendeleza kazi nzuri ianayofanywa na Chama hicho.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa URA SACCOS SACP David Misime alimshukuru Mrajis kwa kutoa hotuba yenye kuonyesha dira na muelekeo chanya wa uboreshaji wa Chama hicho Pamoja na kuimarisha utendaji wa Sekta ya Ushirika nchini. Amesema URA SACCOS itaendelea kusimamia na kutoa huduma bora kwa wanachama wake kwa mujibu wa Sheria, taratibu na Kanuni za Vyama vya Ushirika.





Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: