Raisa Said,Kilindi


Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kuongeza vyanzo vingine vya mapato kwaajili ya bajeti za lishe badala ya kusubiri chanzo kimoja cha mapato ya ndani ya Halmshauri husika.


Ombi hilo limetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Dk Daniel Chochole  wakati Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi kuhusu hali ya lishe katika Wilaya hiyo.


Dk Chochote alisema kuwa endapo Serikali itaongeza vyanzo hivyo vya mapato vitasaidia katika kutekeleza afua mbalimbali za lishe ili waweze kutengeneza afya bora za watoto wenye umri  chini ya miaka mitano katika  makuzi yao.


Mganga  Mkuu huyo alisema kuwa  kumekuwa na changamoto Katika utekelezaji was afua mbalimbali za lishe kutokana na kutegemea Makusanyo kutoka katika vyanzo vya halmshauri.


" kwasasa tumekuwa tukitumia bajeti za lishe  kutoka katika vyanzo vya  mapato vya halmashari"Alisema Dr Chochole nakuongeza kuwa Makusanyo ya Halmshauri kwa miaka hii miwili yamekuwa madogo hivyo kumesabisha changamoto Katika utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe.


Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa Lishe wilani Kilindi Fikiri Adam alieleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha wa 2020/2021 serikali imewatengea kiasi cha milion 40 kwa ajili ya utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe wilayani humo.


Adamu alisema kuwa kwasasa wanaendelea na utekelezaji ikiwemo  kutoa elimu mbalimbali ihusuyo namna Bora ya uaandaji wa  lishe bora  kwa mtoto ili kumuandaa makuzi  yao ya Kila siku.


Hata hiyo lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini mara nyingi mamilioni ya watoto hukosa haki hiyo hususani lishe bora kutokana na sababu mbalimbali. UNICEF inasema hali hiyo  inaweka afya za watoto hatarini na pia njiapanda mustakhbali wao.

Share To:

Post A Comment: