NA THOMAS MACHUPA ,RUVUMA

Wananchi wa kijiji cha Muhuwesi kata ya Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamemshukuru mwekezaji Ruby International Ltd kwa kuwajengea Zahanati ya kisasa ambayo itawasaidia kupata huduma bora za Afya.

Pia wamemuomba mwekezaji kuendelea kuwajengea miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu na miundombinu mingine kwani uwezo wa kufanya hayo anao mkubwa sana.

Akizungumza muwakilishi wa Wazee wa Kijiji hicho  Salim Nampipiru amesema wawekezaji wa madini wamepita wengi katika kijiji hicho lakini hawakufanya maendeleo kama hayo hivyo aendelee kuwa mwokozi wa kijiji kwa kipindi hiki.

Naye Bi Hamida selemani amesema yeye kama mwanamke kwaniaba ya wenzake anaishukuru kampuni ya Ruby kwa kuwavika nguo wanawake kwani walikuwa wanadhalilika nyakati za kujifungua hapo nyuma.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Muhuwesi Iman Ngonyani aliwaomba wananchi kuendelea kumlinda na kumpa sapoti mwekezaji ili awe na moyo wa kuendelea kukisaidia kijiji chao kauli ambayo imeungwa mkono na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru Sizza Marandu ambapo amesema ni wawekezaji wachache wanaokumbuka kufanya maendeleo katika vijiji wanavyowekeza.

Salim Alaudin Hasham ndiye mkurugenzi wa Ruby International Ltd ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa wananchi na kwa kipindi chote atakachokuwepo kijijini hapo ataendelea kusaidia mambo mbalimbali ya kimaendeleo.

Kijiji cha Muhuwesi kimekuwa maarufu kutokana na kutoa madini  ya vito yenye thamani kubwa  ambayo yanatoka kwenye mto muhuwesi unaopita kwenye kijiji hicho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: