Na Mwandishi Wetu,
MSHAMBULIAJI
mpya wa Manchester United ya Uingereza, Cristiano Ronaldo amenza kazi
na Klabu hiyo na kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu Soka
nchini Uingereza (EPL) dhidi ya Newcastle United kwenye ushindi wa jumla
wa bao 4-1 katika dimba la Old Trafford nchini humo.
Ronaldo kwa
mara ya kwanza akivaa Uzi wa Manchester United na wakiwa nyumbani Ngome
Kongwe, alifanikiwa kupata mabao hayo mawili kwa umahiri kabisa katika
dakika ya 45+2’ na dakika ya 62’ ya mchezo huo huku mabao mengine
yakifungwa na Mshambuliaji Bruno Fernandes dakika ya 80’ na Jesse
Lingard dakika ya 90+2’ wakati bao la Newcastle likifungwa na J.
Manquillo dakika ya 56’.
Msimu huu ni msimu mpya kwa Nyota
Cristiano Ronaldo kucheza Man United baada ya awali, mwaka 2003 hadi
2009 wakati timu hiyo ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sir Alex Ferguson
ambapo baadae CR7 alitimkia Real Madrid alipocheza kati ya mwaka 2009
hadi 2018 na alitua Italia katika timu ya Juventus na kucheza kati ya
misimu ya 2018 hadi 2021.
Ni rasmi sasa Cristiano Ronaldo dos
Santos Aveiro maarufu CR7 amerejea tena Manchester United chini ya Kocha
Mkuu Ole Gunnar Solskjær.

Post A Comment: