Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge  akiwasalimia  na kuwapa pole manusura wa chakula  kinachosadikika kuwa na sumu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge  akiwasalimia  na kuwapa pole manusura wa chakula  kinachosadikika kuwa na sumu.
Na Edina Malekela,Singida
Mkuu
 wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewatembelea wananchi 
waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa huo baada kula chakula 
kinachosadikika kuwa na sumu ambapo katika tukio mtoto mmoja  mwenye 
umri wa miaka 7 amefariki dunia huku watu wengine 50 wakinusurika kifo.
Wakazi
 hao wa Kata ya Unyambwa kijiji cha Kisasida katika Manispaa ya Singida 
mkoani Singida walifikishwa hospitalini hapo jana baada ya hali zao kuwa
 mbaya kutokana na kula chakula kilichoandaliwa katika shughuli za 
ufunguzi wa Madrasa kijijini hapo.
Dkt.
 Mahenge amewapongeza madaktari wa Hospitali hiyo kwa jitihada za 
kuhakikisha wananusuru maisha ya wananchi hao ambapo kwa sasa hali zao 
zinaendelea vizuri na kuipongeza Serikali kwa kuweka miundombinu mizuri 
ya huduma katika sekta ya afya.
Ametoa
 wito kwa Viongozi wa Serikali na Dini kuwajibika kikamilifu katika 
kutoa elimu ya namna ya kuandaa chakula pamoja na kusimamia inapotokea 
sherehe mbalimbali kwenye maeneo yao ili kuepuka madhara ya namna hiyo.
Kwa
 mujibu wa Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Banuba Deogratius 
amesema walipokea jumla ya wagonjwa 50,kati yao Wanawake 34 na Wanaume 
16 ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wanaanza kuwaruhusu baadhi yao 
kurudi nyumbani kuendelea na majukumu yao.
Aidha
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella Mutabihirwa amesema 
wanawashikilia washukiwa 7 walioshiriki kuandaa chakula hicho kwa ajili 
ya uchunguzi na tayari wamechukua chakula hicho kwa uchunguzi zaidi.
Katika tukio hilo Kamanda amesema mtoto mmoja mwenye umri wa miaka (7) ambaye amefahamika kwa jina la Fahad Masudi amefariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.



Post A Comment: