Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge (kulia) akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wakati akikagua mradi wa kilimo cha umwagiliaji Itagata Itigi alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kuzungumza na wananchi.

Afisa Kilimo Wilaya ya Itigi Mkinguzi Mgalula akitoa taarifa ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa

      Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, akizungumza katika ziara hiyo.

Muonekano wa miundombinu ya umwagiliaji ya mradi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi John Mgalula akizungumza katika ziara hiyo.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba akizungumza katika ziara hiyo.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi  wakiwa katika kikao cha ndani na mkuu wa mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigikatika kikao cha ndani.
Mkurugenzi wa Hospitali ya St Gaspar iliyopo Itigi mjini, Fr. Justin Boniface akitoa taarifa ya hospitali hiyo  kwa mkuu wa mkoa.
Ukaguzi Hospitali ya St Gaspar ukifanyika.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Itigi wakiwa kwenye ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Manyoni Jumanne Muhanda, akizungumza katika ziara hiyo.
Muonekano wa mashamba ambayo yameshindwa kuendelezwa.
Mhandisi William Kadinda Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkoa wa Singida  akizungumza katika ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagata Salum Mbesi (katikati) akizungumza katika ziara hiyo.
Diwani wa Kata ya Itagata Martin Kapona, akizungumza katika ziara hiyo.
Mkazi wa Kijiji cha Itagata, Mussa Lupia. akizungumza katika ziara hiyo.


Na Dotto Mwaibale, Itigi.


MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge ameagiza uongozi wa wilaya ya Itigi kuitisha kikao cha viongozi wa Kijiji cha Itagata, wananchi na wadau wa kilimo ili kunusuru mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa kijiji hicho ambao Serikali ilitoa Sh. 2 Bilioni kwa ajili ya kuanzisha mradi huo ulioridhiwa na wananchi lakini haufanyi kazi kwa sababu mbalimbali.


Dkt.Mahenge alitoa agizo hilo jana wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kuzungumza na wananchi.

" Ninaagiza muitishe kikao hicho haraka sana na mimi mwenyewe nitakuja, nilipokuwa nasikiliza takwimu za mradi huu za Sh.2.1  Bilioni za ambao haufanyi kazi nimesikitika sana  kwani kuna maeneo wanalia kukosa fursa ya namna hiyo nawaambia kwa uvivu wenu huo mtaendelea kulalamika na kuwa maskini ". alisema Mahenge.

Alisema baada ya kikao hicho ndipo watakapoamua kuona cha kufanya ikiwa ni pamoja na kuwapatia mashamba hayo watu wengine wenye uwezo ya kuyaendeleza baada ya wananchi wanachama wa kilimo cha umwagiliaji waliopewa kushindwa kuyafanyia kazi.

Afisa Kilimo Wilaya ya Itigi Mkinguzi Mgalula akitoa taarifa ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa alisema mradi wa kilimo cha umwagiliaji Itagata una jumla la eneo la  hekta 160 linalofaa kwa kilimo sawa na ekari 400 na kuwa eneo linalofikiwa na miundombinu ya umwagiliaji ni hekta 83.6 sawa na ekari 209.

Alisema mradi huo ni matokeo ya wazo lililobuniwa na wananchi wa kijiji hicho wakati wa zoezi la kubaini fursa na vikwazo vya maendeleo na hatimaye kuingizwa kwenye mpango wa maendeleo ya kilimo cha Kijiji cha Itagata mwaka 2008/ 2009.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu mradi huo ambao umekwaka kuendelea viongozi mbalimbali wananchi na wadau wengine waliunga mkono agizo la mkuu wa mkoa la kuitisha kikao hicho ili kitoe maamuzi ya kuyachukua mashamba hayo na kuwapa watu wengine ambao watakuwa na uwezo ya kuyaendeleza.

Baadhi ya viongozi waliotoa maoni hayo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagata Salum Mbesi, Diwani wa Kata hiyo Martin Kapona, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Manyoni Jumanne Muhanda, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwepo Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo hicho cha umwagiliaji Itagata, Rashid Mfaume, Zena Matonya na Mussa Lupia.

Walitaja baadhi ya sababu  za mradi huo kukwama ni uvivu, ubinafsi na watu kukumbatia mashamba ambayo wanashindwa kuyaendeleza huku wengine wakiyakodisha kwa bei kubwa.

Mussa Lupia alisema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itoa kipaumbele kwa kuwapa kwanza mashamba wananchi wa kijiji hicho walioibua mradi huo lakini wameshindwa kuyaendeleza hivyo analiunga mkono wazo la mkuu wa mkoa la kuitisha kikao hicho ili kitoe maamuzi ya kuwapa watu wengine watakaokuwa na uwezo wa kuyaendeleza kutoka ndani ya kijiji hicho na nje.

Katika ziara hiyo Dkt.Mahenge alitembelea Hospitali ya St Gaspar iliyopo Itigi mjini na kuona huduma kubwa za matibabu zonazofanyika zikiwemo za upasuaji na akatoa wito kwa wananchi mbalimbali kutoka mikoa jirani na Singida kwenda kupata huduma za upasuaji na matibabu mengine badala ya kukimbilia Hospitali zingine kubwa za hapa nchini na kutumia gharama kubwa ambapo pia alizungumza na Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kusisitiza ukusanyaji wa mapato na kutenga asilimia 10 ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: